Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
ULY CLINIC
9 Oktoba 2021, 12:19:04
Sampuli gani huchukuliwa kwa ajili ya kufanya kipimo cha COVID-19 ni damu, makamasi au kinyesi?
Sampuli inayochukuliwa kwa ajili ya kupima COVID-19 huchukuliwa kutoka puani. Taratibu za kimatibabu humtaka kila mtu anayefanyiwa matibabu kuridhia aina ya matibabu aidha yeye mwenyeweau ndugu wa karibu kama mgonjwa hawezi kutoa ridhaa yake. Mhusika huelezwa aina haguzi (options) zote zilizopo kwa ajili matibabu na huchagua inayomfaa. Mfano mtu akitaka kufanyiwa upasuaji anatakiwa kuridhia au unapotaka kutumia njia za uzazi wa mpango. Hata hivyo, Sema kwa baadhi maeneo huwa ngumu kutekeleza takwa hili la kitaaluma kutokana na ufinyu wa muda, wingi wa wagonjwa n.k. Lakini ni lazima mtaalamu wa afya kabla ya kumtibu mtu umpe options zote umwelezee kwa undani kila aina ya matibabu na faida yake na hasara yake ili yeye achague kulinga na uwezo na alivyoamua. Mara nyingi ridhaa nyingi huwa haziwekwi kwenye maandishi, hivyo hii imeboreshwa kwa ajili ya kuweka kumbukumbu.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021, 12:27:42
Rejea za mada hii