top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

9 Oktoba 2021, 12:35:10

Uchanganyaji wa chanjo za COVID-19

Kama mtu amechanjwa chanjo ya Pfizer (dozi ya kwanza) anaweza kuchoma Janssen (J&J) dozi ya pili au anatakiwa achome zinazofanana? (kama J&J achome hizo au kama ni Pfizer achome Pfizer zote)

Chanjo ya Janssen hutolewa kwa dozi moja tu wakati Pfizer hutolewa kwa dozi mbili. Utafiti nchini Uingereza (Com-CoV Study) umeonyesha ufanisi mtu akipokea chanjo ya kwanza ya AstraZeneca ikifuatiwa na chanjo ya pili ya Pfizer. Tafiti bado zinaendelea ili kubaini ufanisi na madhara ya uchanganyaji wa aina tofauti za chanjo. Kwa ushahidi uliopo hadi sasa, inashauriwa kutumia aina ile ile ya chanjo.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021, 12:45:19

Rejea za mada hii

bottom of page