Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
13 Novemba 2021, 07:39:46
Umri gani uanze kusafisha meno ya mtoto?
Meno ya mtoto yanapaswa kusafishwa mara meno ya kwanza yatakapoota. Kitambaa safi safi chenye unyevu ili kinashauriwa kutumika kusafisha meno na eneo la mbele ya ulimi kila baada ya kula na wakati wa kulala.
Tumia kitambaa safi chenye unyevu ili kusafisha meno ya kwanza ya mtoto mara yatakapoonekana kila baada ya kula na wakati wa kulala.
Madaktari wa meno wa watoto hushauri matumizi ya mswaki maalumu wa mtoto uliolowekwa kwenye maji utumike kusafisha meno ya mtoto. Kiasi cha dawa ya meno kinatakiwa kisizidi punje ya mchele na wakati wa kusafisha meno nguvu haitakiwi kutumika.
Je unaweza safisha fizi pia kwa mswaki?
Hapana!
Haishauriwi kusafisha meno ya mtoto kwa kutumia mswaki hata kama ni mswaki wa mtoto. Inashauriwa kutumia kitambaa safi kilicho na unyevu ili kusafisha meno ya mtoto ili kuhakikisha kuwa fizi zake zinakuwa kwenye hali ya usafi.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
13 Novemba 2021, 09:56:35
Rejea za mada hii
American Academy of Pediatric Dentistry. Frequently asked questions (FAQ).
American Academy of Pediatrics. Brushing up on oral health. Never too early to start. Imechukuliwa 13.11.2021
What to Expect the First Year, 3rd edition, Heidi Murkoff.
WhatToExpect.com. Baby Teeth Chart. Types and Order of Appearance. Imechukuliwa 13.11.2021
WhatToExpect.com. When Do Babies Start Teething?. Basics, Symptoms and Signs. Imechukuliwa 13.11.2021