top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D & Dkt. Benjamin L, M.D

23 Julai 2023, 14:47:50

Unaweza kuambukizwa VVU kwa kung'atwa na mwathirika?

Unaweza kuambukizwa UKIMWI kwa kung'atwa na mwathirika?

Kung'atwa na mwathirika wa VVU kunaweza kupelekea kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Ripoti zilizopo zinaonyesha kuwa waliong'atwa na kupata majeraha makubwa yanayotoa damu mwilini ndio waliopata maambukizi. Njia hii hata hivyo inachangia kwa nadra sana maambukizi ya VVU na watu waliowengi wenye majeraha madogo huwa hawapati maambukizi.


Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yanaweza kutokea endapo kidonda kimekutana na majimaji ya kidonda, damu au majimaji ya uke, shahawa na njia ya haja kubwa kutoka kwa mwathirika.


Endapo umeng'atwa na mwathirika wa VVU na unahisi hatari ufanye nini?

Kama umeng'atwa na mwathirika, nawa kwa maji tiririka ya kutosha kusafisha kidonda kwa dakika 5 hadi 10 kisha fika hspitali zaidi kwa ushauri na kuanzishiwa PEP kama itaonekana inafaa. Kama kidonda kinatoka damu, kwa muda mrefu, hakikisha unatumia njia ya kuizuia isitoke zilivyoelezewa sehemu nyingine katika tovuti hii.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

12 Agosti 2023, 08:48:12

Rejea za mada hii

  1. HI. gov. How Is HIV Transmitted?. https://www.hiv.gov/hiv-basics/overview/about-hiv-and-aids/how-is-hiv-transmitted/. Imechukuliwa 23.07.2023.

  2. ULY CLINIC. Virusi vya UKIMWI. https://www.ulyclinic.com/virusi/Virusi-vya-UKIMWI. Imechukuliwa 23.07.2023.

  3. Cresswell FV, et al. A systematic review of risk of HIV transmission through biting or spitting: implications for policy. HIV Med. 2018 Apr 23;19(8):532–40. doi: 10.1111/hiv.12625. Epub ahead of print. PMID: 29687590; PMCID: PMC6120498.

  4. Patil PD, et al. Managing human bites. J Emerg Trauma Shock. 2009;2:186–190. doi: 10.4103/0974-2700.55331.

  5.  Cresswell FV, et al. A systemic review of risk of HIV transmission through biting spitting: implications for policy. HIV Med. 2018;19:532–540. doi: 10.1111/hiv.12625.

bottom of page