top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Imeboreshwa:

15 Julai 2025, 07:10:50

Vipele Fodisi: Chanzo, Dalili na Matibabu

Vipele Fodisi: Chanzo, Dalili na Matibabu

Swali la msingi

“Shikamoo Daktari, nimekuwa na vipele vidogo vidogo kwenye uume kwa zaidi ya miezi saba sasa. Haviumi wala kuwasha lakini vimejaa sehemu nyingi, vinaonekana kama mafuta au chembechembe ndogo za rangi ya ngozi. Nilidhani ni maambukizi ya ngono lakini vipimo havijaonyesha tatizo. Je, huu ni ugonjwa gani na unatibika?”


Majibu

Vidoa Fodisi ni nini?

Fodisi spot( Fodyce Spots) hufahamika pia kama vidoa Fodisi au vipele Fodisi ni vipele vidogo visivyo na maumivu vinavyotokea kwenye midomo hasa mdomo wa juu, sehemu za siri kama mashavu ya uke, uume au korodani, au maeneo mengine ya ngozi. Ingawa vinaweza kutia wasiwasi, si ugonjwa wa kuambukiza wala hatari kiafya. Makala hii inaeleza kwa kina chanzo chake, tofauti na magonjwa mengine, na njia za kutuliza au kutibu kwa usalama.


Fodisi ni tezi za mafuta ambazo zipo juu ya ngozi kuliko kawaida, lakini hazijaunganishwa na nywele. Kwa kawaida, kila mtu anao, lakini kwa baadhi hujitokeza kwa wazi zaidi.


Dalili zake ni zipi?

Dalili

Maelezo

Rangi ya ngozi au njano

Bila uwekundu au kuvimba

Hakuna maumivu

Tofauti na fangasi au vipele vya bakteria

Haviwashi

Hayana usumbufu, isipokuwa kwa muonekano

Haijaambatana na harufu

Tofauti na maambukizi ya zinaa

Vinaweza kuonekana kwa wingi

Hasa kwa wanaume kwenye uume au korodani


Je, husababishwa na nini?

  • Sio maambukizi

  • Sio ugonjwa wa zinaa (STI)

  • Ni mabadiliko ya kawaida ya ngozi, huweza kuonekana zaidi wakati wa kubalehe au kwa watu wenye ngozi yenye mafuta mengi.

Visivyohusika:

  • Sio HPV

  • Sio fangasi

  • Sio herpes

  • Sio kaswende


Tofauti na magonjwa mengine

Kipengele

Vidoa vya Fodisi

Herpes / Fangasi / STIs

Maumivu

Hakuna

Ndio, mara nyingi

Kuwasha

Hapana

Sana sana

Kubadilika kwa rangi

Hupotea taratibu

Huwa na wekundu au vidonda wazi

Harufu au usaha

Hapana

Ndio, mara nyingine

Kuambukiza

Hapana

Ndio


Matibabu au utulizaji

Kwa kuwa Vidoa Fodisi si ugonjwa, havihitaji matibabu, isipokuwa kwa sababu ya kisaikolojia (muonekano).


Hatua za kuchukua nyumbani
  • Epuka kukandamiza au kuvibinya – huongeza uwezekano wa kuleta maambukizi

  • Safisha eneo kwa sabuni nyepesi isiyo na kemikali

  • Epuka mafuta au krimu nzito – huchochea kuonekana zaidi


Matibabu ya kitaalamu (kwa wanaohitaji kuviondoa)

Njia ya Matibabu

Maelezo

Tiba ya mwanga wa leza

Kufuta vipele kwa mwanga maalum wa leza

Epasuaji kwa njia ya umeme

Kuchoma seli kwa umeme mdogo

Upasuaji mdogo wa kutoboa vipele

Kutoboa vipele kwa vifaa maalum – Ni ghali na hupatikana sehemu maalum

Krimu jamii ya Retinoid

Hutumiwa chini ya usimamizi wa daktari wa ngozi

Tiba hizi zinaweza kuwa ghali na wakati mwingine zinaweza kuacha makovu. Ni muhimu kushauriana na daktari wa ngozi kabla ya kuanza.

Je, vinaweza kuondoka vyenyewe?

Ndiyo, mara nyingi hupungua taratibu bila matibabu. Kwa baadhi ya watu, huendelea kuwepo maisha yote bila shida yoyote ya kiafya.


Wakati wa kumwona daktari?

Onana na daktari endapo;

  • Vipele vimebadilika ghafla (rangi, ukubwa, umbile, au vimeanza kuuma)

  • Vinaambatana na vipele vingine vinavyosambaa

  • Una mashaka kuhusu hali ya ngozi yako

  • Unapata msongo wa mawazo au aibu ya muonekano


Hitimisho

Vidoa Fodisi ni vipele vya kawaida visivyo na madhara, na si ugonjwa wa zinaa. Ingawa vinaweza kuleta wasiwasi wa muonekano, havihitaji matibabu isipokuwa kwa sababu za kisaikolojia au urembo. Kushauriana na daktari wa ngozi ni njia salama ya kupata uhakika na utulivu wa akili.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

15 Julai 2025, 07:10:50

Rejea za mada hii

  1. James WD, Elston D, Treat JR, Rosenbach M. Andrews’ Diseases of the Skin: Clinical Dermatology. 13th ed. Elsevier; 2020.

  2. Satter EK, Grossman ME. Fordyce spots. In: Fitzpatrick's Dermatology. 9th ed. McGraw-Hill Education; 2019.

  3. Jha AK, Sonthalia S. Fordyce spots: a review of pathophysiology and management. J Cutan Aesthet Surg. 2020;13(1):5–9.

  4. Al Aboud A, Nigam PK. Fordyce spots. [Internet]. StatPearls Publishing; 2024. Available from: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537291/

  5. American Academy of Dermatology Association. Fordyce spots. [Internet]. 2023. Available from: https://www.aad.org

  6. Lippincott Illustrated Reviews: Dermatology. Wolters Kluwer; 2019.

bottom of page