Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
9 Oktoba 2021, 07:23:47

Kwanini wanaongoza kuvunja maelekezo ya Wizara ni viongozi wenyewe tena wakubwa?
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa mwongozo wa njia za kutumia ili kujikinga dhidi ya maambukizi na vile vile kuzuia usambaaji wa kirusi kinachosababisha ugonjwa wa COVID-19. Muongozo huu unatakiwa ufuatwe na watu wote bila kujali kazi wanayofanya, cheo walichonacho kazini, kabila, rangi na dini ya mtu. Watu wote wanashauriwa kuchukua tahadhari kwa;
Kuvaa barakoa
Kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au
Kutumia vipukusi
Kuepuka mikusanyiko
Kuchoma chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021, 09:16:37
Rejea za mada hii
https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019/question-and-answers-hub. Imechukuliwa 09.10/2021