top of page

Imeandikwa na daktari wa ULYCLINIC

​

​

Keloid ni uvimbe katika ngozi ya sikio ama sehemu nyingine ya mwili, husababishwa na kukua sana kwa kovu pasipo kuthibitiwa. Ngozi hupona kwa kutengeneza kovu baada ya kuchanika ama kuumia na kwa mara ya kwanza kovu huwa na rangi nyekundu(kwa watu weupe) na muinuko mdogo. Mda unavyopita kovu hupungua na kupoteza mwinuko huo

​

Kwa bahati mbaya, wakati mwingine makovu huweza hukua sana na kutengeneza kovu gumu au laini na kusambaa zaidi ya eneo lililoathirika au chanika. Kwa kawaida makovu haya yanayoitwa keloid huwa yanawasha na kuuma kwa baadhi ya watu

 

 

Nini husababisha keloid?

​

Hakuna anayefahamu kwanini makovu haya yanatokea, ingawa baadhi ya watu huwa hawapati makovu haya kabisa, wanaopata makovu haya kufuatiwa na hali mbalimbali kama kujikata, kungatwa na mdudu, kupata michubuko ya ngozi ama baada ya kupata chunusi. Mara nyingi makovu haya hutokea maeneo ya masikio, mgongoni, kifuani na mabegani kuliko maeneo mengine ya mwili.

Wa afrika (watu wenye ngozi nyeusi) hupata makovu haya ya keloid kwa kiasi kikubwa sana kuliko watu wa mataifa mengine, ingawa kila mtu anaweza kupata makovu haya. Makovu ya keloid huwa haya badiliki kuwa saratani

​

Matibabu

Matibabu ya keloid ni magumu, ingawa kama mtu akizingatia yanaweza kuondoka kabisa 

​

Matibabu yapo ya aina tofauti ikiwa pamoja dawa na upasuaji

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushuei kutoka kwa daktariwako ka bla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya.

​

Pata tiba na dawa kutoka ULY CLINIC mahali popote ulipo kwa kupiga simu kwa namba zilizo chini ya tovuti hii au bonyeza hapa

​

Toleo la 2

​

Imeboreshwa mara ya mwisho 13.08.2020

​

Rejea za mada hii,

​

  1. Hutchingson text book of internal medicine chapisho 20

  2. ABCs of dermatology toleo la 4, 2003

  3. Absolute dermatology reviewna Hugh Morris Gloster, na wengine

makovu ya keloid matibabu-ulyclinic.jpg
bottom of page