Imeandikwa na ULY CLINIC
Matibabu ya magonjwa ya zinaa wakati wa ujauzito
Magonjwa mengi ya zinaa huambatana na madhara makubwa kwa mtoto na mama wakati wa ujauzito. Wanawake wanatakiwa kufanya vipimo uchunguzi kabla na wakati wa ujauzito ili kutambuliwa na kutibiwa ili kuzuia madhara hayo. Hili ni pendekezo kutoka kwenye mashirika mengi ya kiafya kama WHO na CDC.
​
Maambukizi yanayopaswa kupimwa mapema ni kama maambukizi ya kisonono, kaswende, maambukizi ya kirusi che herpes, na hepatitis B wakati wa kuanza kliniki.
Matibabu ya magonjwa ya zinaa wakati wa ujauzito endapo hakuna umakini inaweza kusabisha pia madhara kwa mama na mtoto. Hata hivyo magonjwa ya zinaa yaliyoorodheshwa hapo juu yanatakiwa kutibiwa ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Baadhi ya dawa zinazotumika katika matibabu ya magonjwa ya zinaa katika ujauzito ni;
-
Azithromycin
-
Ceftriaxone
-
Acyclovir
-
Penicillin
-
Metronidazole
-
Amoxicillin
-
Cefixime
-
Valacyclovir
-
Benzathine penicillin G
Baadhi ya magonjwa ya zinaa mara baada ya kuanza matibabu mgonjwa anatakiwa kufanya vipimo ili kuangalia endapo matibabu yamefanikiwa.
Matibabu pia huhusisha kutibu watu ambao umeshiriki nao au ambao unaendelea kushiriki nao
Kumbuka kila dawa ina matumizi yake kutibu aina fulani ya ugonjwa wa zinaa. Wasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa maelezo zaidi na tiba kupitia namba za simu chini ya tovuti hii au kwa kubonye
-
BARBARA A. MAJERONI, MD etal. Screening and Treatment for Sexually Transmitted Infections in Pregnancy. https://www.aafp.org/afp/2007/0715/p265.html#. Imechukuliwa 7.1.2021
-
M R Cavenee etal. NCBI. Treatment of gonorrhea in pregnancy. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/8416458/. Imechukuliwa 7.1.2021
-
R M Ramus etal. A randomized trial that compared oral cefixime and intramuscular ceftriaxone for the treatment of gonorrhea in pregnancy. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/11568790/. Imechukuliwa 7.1.2021
-
I Portilla etal. Oral cefixime versus intramuscular ceftriaxone in patients with uncomplicated gonococcal infections. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/1534422/. Imechukuliwa 7.1.2021
-
CDC. Bacterial Vaginosis. https://www.cdc.gov/std/tg2015/bv.htm. Imechukuliwa 7.1.2021
-
CDC. Treatment of Chlamydial Infections in pregnancy. https://www.cdc.gov/std/tg2015/chlamydia.htm. Imechukuliwa 7.1.2021