top of page

Mazoezi ya kunyoosha mgongo ili kupunguza maumivu

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

Makala hii inatolewa hapa kwa malengo ya kukupa taariza za elimu tu. Kama ukipata shida dhidi ya mazoezi haya au ugumu wa kufanya mazoezi haya, acha mara moja na wasiliana na mtaalamu wa afya wako. Wasiliana na mtaalamu wa afya wa mazoezi ili akuambie mazoezi kulingana na hali yako ya kiafya

Kabla ya kuanza mazoezi unatakiwa unatakiwa kuchagua mazoezi sahihi kwa ajili yako

Wataalamu wa maumivu wanakubali kwamba kuchagua mazoezi sahihi huweza kupunguza maumivu sugu ya mwili. Mazoezi na kazi za kushugulisha mwili zinaweza kusaidia kutojirudia kwa maumivu hapo mbeleni. Mazoezi haya yatakufanya upone haraka na kurudia hali yako ya awali. Kumbuka ni vema kutathmini maumivu yako wakati unafanya mazoezi. Endapo utapata maumivu zaidi au ugumu kifanya haya mazoezi, acha mara moja na  wasiliana na daktari wako

Dalili unazotakiwa kuwa makini nazo

Dalili ya kwamba mazoezi ya mgongo hayakusaidii

 • Endapo maumivu yanahama kutoka katikati ya mgongo

 • Maumivu yanahamia kwenye makalio

 • Maumivu yanayohamia kwenye mguu

Dalili ya kwamba mazoezi ya mgongo yanakusaidia

 • Maumivu yanaondoka kwenye miguu

 • Maumivu yanahamia zaidi katikati ya mgongo

 • Unaweza kujishughulisha kwa kazi nyingi ukiwa na maumivu kidogo

Dalili za kwamba mazoezi ya kuondoa maumivu ya shingo hayakusaidii

 • Maumivu yanaondoka kwenye shingo kuelekea sehemu nyingine

 • Maumivu kuhamia kwenye mabega

 • Maumivu kuhamia kwenye mikono

Dalili za kwamba mazoezi ya kuondoa maumivu ya shingo yanakusaidia

 • Maumivu yanaondoka kwenye mkono wote

 • Maumivu utahisi zaidi katikati ya shingo

 • Unaweza kufanya kazi zako nyingi ukiwa na maumivu kiasi

Mazoezi haya husabahisha ganzi na miguu kuchomachoma hupotea, lakini hupotea taratibu kuliko maumivu ya mgongo. Achana na mazoezi mara moja endapo mazoezi haya hayakusaidii au endapo maumivu yanazidi maradufu. Endelea na mazoezi ambayo yanakusaidia tu.

Mazoezi ya aerobic

Mfano kutembea, kuendesha baiskeli,kuogelea yanatakiwa kufanyika pia, malengo yakiwa kufanya mazoezi angalau kwa dakika 30 kwa siku kwa mda wa siku tano za wiki. Endapo unaweza kufanya mazoezi mda mrefu zaidi unaweza kuendelea. Kama huwezi kufanya mazoezi haya hapa mwanzoni achana nayo utafanya baadae baada ya kuweza mazoezi haya yaliyozunyumziwa hapa. Kusoma zaidi kuhusu mazoezi ingia kwenye sehemu ya chakula na mazoezi.

 

Kuendelea kusoma jisajili kwa email yako sahihi tu, pia unaweza kuweka application ya uly clinic kutoka google play store ili kuanza kupokea vidokezo muhimu vya kiafya

Utangulizi
Dalili
Aina ya mazoezi
bottom of page