top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

4 Juni 2020 11:44:14

Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu na kujifungua
Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu na kujifungua
Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu na kujifungua
Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu na kujifungua

Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu na kujifungua

Katika kipindi uchungu unaanza hadi kipindi unajifungua, masaa kadhaa yatapita. Kwa mama ambaye anaujauzito wa kwanza inaweza kuchukua muda wa masaa 11 toka uchungu umeanza mpaka kujifungua endapo uzazi ni wa kawaida. Kuna aina mbalimbali za mapozi ambayo mtu anaweza kukaa wakati wa uchungu.


Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu


 • Mfano pozi ni kama kwenye picha ambayo ni

 • Kusimama huku umeegamia ukuta au kumwegamia mtu mwingine aliye karibu nawe kama upo naye na kama inavyoonekana kwenye picha namba 1b na c

 • Kukaa kichura chura kama inavyoonekana kwenye picha namba 2b

 • Kupiga magoti kama inavyoonekana katika picha namba 1d.


Mara ngapi natakiwa fanya mazoezi kwenye mapozi ya ujauzito?


Fanya mazoezi ya kukaa kwenye mapozi haya mara nyingi uwezavyo ili ikifika wakati wa uchungu uweze kuyatumia kirahisi.


Mapozi mengine ya kujifungua ni yapi?


Pozi jingine ni kukaa kifudifudi kwa kupiga magoti huku umelalia mto na kusambaza miguu yako ili kufanya tumbo lako liwe katikati ya miguu kama inavyoonekana kwenye picha namba 2a na d.


Nini faidia za kukaa mapozi maalumu kwa mjamzito?


Mapozi haya yanakufanya wewe ujusikie vema na kumpa nafasi mtoto tumboni nafasi nzuri ya kupita kwenye nyonga ili ujifungue kirahisi.

Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.

ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021

Rejea za mada hii:

 1. American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020

 2. National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020

 3. National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020

 4. https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020

 5. Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020

 6. Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020

 7. Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020

 8. NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020

 9. Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020

bottom of page