top of page

Mwandishi:

ULYCLINIC

30 Aprili 2020 08:02:41

Mazoezi wakati wa ujauzito
Mazoezi wakati wa ujauzito
Mazoezi wakati wa ujauzito
Mazoezi wakati wa ujauzito

Mazoezi wakati wa ujauzito

Mazoezi kipindi cha ujauzito hushauriwa sana na wakunga yafanyike wakati wote haswa kipindi cha ujauzito, leba na kijifungua. Sababu kuu ya kwanini mazoezi haya yafanyike zaidi kuliko maandalizi mengine ya uzazi, ni kwa sababu ya umuhimu wake mkubwa kwenye afya ya mama na mtoto kipindi chote cha ujauzito, leba na kujifungua.


Kujifunza mambo haya yatafanya ujauzito wako usikuchoshe na ujiamini zaidi. Mara baada ya kusoma Makala hii utaanza kulala vizuri, kuhisi una nguvu nyingi, kujiamini na kuwa na matarajio makubwa.


Mfano maungio ya mwili wako yatakuwa laini, utakuwa na nguvu nyingi kwenye misuli ya uzazi zinazohitajika wakati wa uchungu na kujifungua. Utaweza kuimarisha na kukuza misuli ya sakafu ya nyonga ili kuweza kubeba mtoto vizuri. Pi kufahamu kuhusu pozi mbalimbali za ujauzito zitakusadia kumlaza mtoto tumboni katika pozi zuri na asilia na kumfanya mtoto akue vizuri tumboni.


Umuhimu wa makala ya mazoezi ya wajawazito


Makala hii itakusaidia kuufurahia muda wako wa mazoezi na utajisikia vizuri sana. Kwa nyongeza, utaondokwa na msongo wa mawazo kwani utafundishwa namna ya kujipa muda maalumu wa kuwa peke yako, hii ni muhimu kwa kila mama mjamzito. Unapofanya mazoezi haya utajigundua kwamba unaanza kupumua vizuri na kwa kina bila kuishiwa pumzi na hivyo kuongeza kiwango cha hewa ya oksjeni kinachohitajika kwako na mtoto tumboni. Utapumua nje hewa chafu ya kabon dayoksaidi na sumu zingine ambazo haitakiwi kwako na kwa mtoto.


Makala hii pia itakupa taarifa zaidi za namna sahihi ya kujibeba mwenyewe, namna ya kutembea na namna ya kulala kwenye pozi lenye uhuru zaidi. Utajikuta unakuwa fanisi kwenye kazi mbalimbali na utafurahia mwenyewe endapo utafuata maelekezo sawasawa. Wakunga na nesi wanasisitiza mazoezi wakati wa ujauzito kwa sababu ya umuhimu wake. Kutokana na tafiti za kisayansi, waliona kwamba unapofanya mazoezi husaidia mimba ikuwe vema, leba na uzazi itokee kwa urahisi, kuimarisha upumuaji na misuli ya nyonga kwa uzazi salama.


Wakati gani unapaswa kuanza mazoezi?


Mimba inapofikisha wa miezi sita, unatakiwa uwe umeashaanza kufanya mazoezi haya. Mtoto tumboni atapata mabadiliko ya kifiziolojia yanayohusiana na uzazi. Mtoto atakaa kwenye pozi sahihi ili uweze kujifungua kwa njia ya kawaida (njia ya uke). Utaanza kusikia mapigo ya moyo ya mtoto unapokuwa mwezi wanne wa ujauzito na kuendelea. Mtoto ataongeza mapigo kwa jinsi siku zinavyoenda.


Kwanini usome makala hii na kuzingatia kwenye ujauito wako?


Makala hii imeandikwa na wataalamu wa afya, kutokana na tafiti za kisayansi zilizofanyika na hivyo ni ya kuaminika.

Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.

ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021

Rejea za mada hii:

  1. American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020

  2. National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020

  3. National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020

  4. https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020

  5. Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020

  6. Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020

  7. Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020

  8. NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020

  9. Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020

bottom of page