top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

2 Juni 2020 12:35:29

Mazoezi ya kuimarisha misuli ya Tumbo
Mazoezi ya kuimarisha misuli ya Tumbo
Mazoezi ya kuimarisha misuli ya Tumbo
Mazoezi ya kuimarisha misuli ya Tumbo

Mazoezi ya kuimarisha misuli ya Tumbo

Kabla hujaanza kufaya mazoezi haya, ni vema ukaelewa kwanza taarifa zifuatazo kuhusu kuitenganisha misuli ya tumbo. Wakati wa ujauzito, mstari mweusi unaoitwa linea alba hujitokeza katikati ya mwili nje ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya homoni kwa mama mjamzito yanayoletwa na ujauzito. Msatri huu huligawa tumbo kwenye sehemu mbili iznazofanana. Homoni za ujauzito husababisha eneo katikai ya maeneo makubwa haya mawili kulainika ili kuruhusu ukuaji wa mtoto tumboni. Endapo eneo hili likirainika na kutanuka zaidi ya kawaida, huweza kutengana. Utengano huu hutokea bila wewe kujua na hausababishi maumivu yoyote yale. Hata hivyo utapata maumivu ya mgongo, na kama ulikuwa nayo tayari yatazidi zaidi.


Misuli ya tumbo ya tumbo inatakiwa kuwa na nguvu sahihi ili kuweza kubeba tumbo na kufanya kazi zake za kukupa pozi sahihi la mgpngo. Endapo hili halitatokea, misuli ya mgongo itafanya kazi ya ziada kurejesha pozi sahihi la mgongo na hivyo kukupelekea kupata maumivu ya mgongo.


Namna gani unaweza kujua misuli ya tumbo imetengana?


Unaweza kuangalia na kujua endapo misuli ya tumbo imetengena muda wowote ule kwa kutumia maelezo yafuatayo;


 • Lalia mgongo kisha kunja magoti yako huku kanyagio likiwa chini ya arthi kisha,

 • Nyanyua kichwa chako taratibu mpaka kidevu kiguse kifua chako wakati miguu yako ipo aridhini

 • Kwa kutumia mkono mmoja tizama kuweo kwa uwazi kwenye eneo la mstari wa linea alba (Uwazi huanza kuonekana ndani ya miezi michache ya ujauzito)

 • Unaweza kuhisi eneo laini kati ya misuli ya tumbo kwenye mstari mwesu lenye upana wa vidole viwili au vitatu


Baada ya kutambua udhaifu wa misuli ya nyonga ufanyaje?


Endapo utengano wa misuli unaonekana au umehisi kwa vidole vyako, hii inamaanisha kuna udhaifu kwenye misuli hiyo ya tumbo hivyo unahitajika kuifanyisha mazoezi ili irejee kwenye hali yake ya kawaida. Misuli hii huwa na umuhimu sana wakati wa kusukuma mtoto. Baadhi ya mazoezi unayowez akufanya yameonyeshwa kwenye picha namba 1 hadi nne na kuelezewa katika maelezo haa chini


Zoezi la kuimarisha misuli ya tumbo kwa mjamzito

Tazama picha namba moja


Mazoezi ya kuimarisha misuli ya mgongo


Ili kuweza kuimarisha mkunjo asilia wa mgongo fanya zoezi kama linavyoonekana kwenye picha namba moja. Zoezi hili licha ya kuimarisha misuli ya mgongo, huimarisha misuli ya tumbo pia. Kufanya zoezi hili;


 • Lalia mgongo wakati umekunja magoti huku kanyagio likigusa ardhi.(kama kwenye picha namba moja

 • Weka mkono mmoja chini ya mgongo na mwingine juu ya tumbo

 • kaza misuli ya tumbo na sukuma kiuno chini ya mkono wako hesabu 1,2,3 kabla ya kupumzika na kupumua kawaida. Rudia zoezi hili mara tano kwa siku. Unawez akuongeza idadi ya zoezi mara nyingi uwezavyo. Zoezi hili unaweza ukalifanya ukiwa umesimama pia.


Ili kuendelea kwenye zoezi la picha namba 2, 3 kama inavyoonekana katika picha hizo, kaa pozi la picha namba 2.


Mjamzito yupi anaruhusiwa kufanya mazoezi ya kuimarisha mizuli ya tumbo?


Zoezi la 1,2 na 3 linatakiwa kufanyika kwa wamama wajawazito ambao wapo kwenye miezi minne ya kwanza ya ujauzito.


Zoezi namba 4 pia husaidia kuondoa maumivu ya mgongo, hata hivyo mazoezi haya husaidia kukurejesha kwenye umbo lako la awali ukiyafanya mara baad aya kujifungua

Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.

ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021

 1. American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020

 2. National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020

 3. National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020

 4. https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020

 5. Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020

 6. Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020

 7. Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020

 8. NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020

 9. Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020

bottom of page