top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

1 Mei 2020 14:52:34

Pozi sahihi wakati wa ujauzito 1
Pozi sahihi wakati wa ujauzito 1
Pozi sahihi wakati wa ujauzito 1
Pozi sahihi wakati wa ujauzito 1

Pozi sahihi wakati wa ujauzito 1

Moja ya kitu muhimu katika afya ya ujauzito ni kukaa pozi sahihi. Kukaa pozi sahihi husaidia kupunguza maumivu ya shingo na nyuma ya mgongo na kuondoa uchovu wa kupitiliza. Hata hivyo wakati wa ujauzito mabadiliko ya kifiziolojia mwilini hutokea na huchangia mwili wa mama usikae katika mpangilio mzuri.


Maelezo katika sehemu hii yatakusaidia kukaa katika pozi la kiafya kipindi chote cha ujauzito, wakati wa kukaa, kulala na kusimama. Ukiwa na pozi sahihi, mwanao tumboni anakuwa kwenye pozi la utulivu na kujihisi vizuri pia husaidia kichwa cha mtoto kiingie vema kwenye tundu la uzazi na ujifungue kwa wepesi. Hii hupelekea mama kufurahia kipindi cha ujauzito na kupata matokeo mazuri ya mimba.


Madhara ya ujauzito kwenye mhimiri wa mwili


Pozi la mhimiri wa mwili hubadilika kutokana na ujauzito, hii ni jambo la asilia na ni kwa sababu misuli ya tumbo hutanuka jinsi mtoto anavyokuwa. Misuli ya tumbo kipindi hiki hushindwa kusinyaa vema ili kuleta mpangilio mzuri wa mgongo. Ili kupinga upinde mkubwa unaotokea nyuma ya mgongo katika kipindi hiki, ni vema ukatembea ukiwa umenyooka ili kwamba masikio, mabega, mgongo na nyonya viwe kwenye mpangilio asilia.


Namna ya kuhimarisha muhimili wa mwili


Ili kuweza kuhimirisha muhimiri wa mwili wako wakati umesimama, vitu vifuatavyo vinaweza kuwa muhimu


 • Hakikisha nyonga yako imekaa pozi sahihi muda wote, hii itasaidia kupinguza upinde wa mgongo wa chini

 • Kaza misuli ya tumbo na makalio ili ifanye kazi asilia ya kuimarisha mgongo

 • Ingiza ndani kidevu chako, yaani kielekee karibu na kifua na masikio yako yawe kwenye msitari mnyoofu na mabega

 • Zuia kuvaa viatu vyenye visigino virefu, viatu hivi husababisha uzito wako uelekee zaidi mbele ya mwili. Vaa viatu vyenye visigino vifupi na vinavyokupa uhuru

 • Unapofanya kazi yoyote wakati umesimama kwa kipindi kirefu kama vile kupiga pasi, kuosha vyombo, hakikisha umeweka mguu mmoja juu ya stool au jiwe au kiti kifupi, au kaa kwenye stuli ndefu, hii itazuia mgongo wako kupindia mbele.

 • Usikunje nne kama kwenye picha namba 3 unapokuwa umekaa kwenye kiti au kukunja miguu yako, hii itasaidia damu kupita vema

 • Ukiwa umekaa kaa kama inavyoonekana kwenye picha namba 4 kwa kuweka miguu chini ya stuli fupi


Mambo ya kutofanya ili kutoharibu muhimili wa mwili wako


Zuia kuupa upinde mgongo wako na pozi lolote lile la kujikuunjia mbele. Simama wima na legeza mabega yako, fanya hivi kwa namna yoyote ile na unapotembea tembea ukiwa unapishanisha mikono yako mmoja baada ya mwingine.

Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.

ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021

 1. American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020

 2. National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020

 3. National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020

 4. https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020

 5. Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020

 6. Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020

 7. Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020

 8. NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020

 9. Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020

bottom of page