top of page

Dawa ya mwanamke kufika kileleni| ULYCLINIC

Updated: Sep 16, 2021


Dawa ya kumfikisha mwanamke kileleni haraka


Wanawake wengi huwa wanafika kileleni kwa shida sana kwa kila wanapojamiana na wapenzi wao. Inawezekana mmekuwa na muda wa kutosha kufanya maandalizi yaani romance lakini bado ukaacha kufika kileleni au ukachelewa licha ya juhudi zote alizofanya mpenzi wako.


Hata hivyo baadhi ya wanawake hawajawahi kufika kileleni na hawajua ni nini maana ya kufika kileleni.


Kufika kileleni ni nini?


Kufika kileleni kwa jina jingine la orgasm. Orgasm ni hisia ya raha kali ambayo hutokea karibu na wakati wa mwisho wa shughuli za ngono na kwa wakati mwingine huitwa kupizi au kufikia kilele. Watu wengi wakati wanashiriki huweza kupata orgasms na wengine hupata kwa shida au kutopata kabisa.


Wakati wa orgasm mapigo ya moyo wako hupiga kwa haraka zaidi na pumzi hubadilika. Endapo unapata orgasm ya uke au kisimi, hisia kali ya raha hufuatiwa na mvutano wa misuli ya maeneo ya uke hutokea.


Baadhi ya wanawake humwaga majimaji wakati wa orgasm. Majimaji haya huwa meupe na hutokea kwenye tezi skenes’ zilizo karibu na mrija wa urethra wakati wa msisimuko mkali wa orgasm.


Endapo unaendelea kushiriki ngono baada ya kupata orgasm, unaweza kupata orgasm nyingine endapo unaendelea kusisimuliwa.


Zipo sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha usifike kileleni kirahisi, sababu hizo zimeandikwa katika makala nyingine bonyeza hapa kusoma.


Makala hii imejikita kuzungumzia namna gani unaweza kufanya au ni nini utumie ili ufike kileleni kwa haraka zaidi.


Ni nini unaweza kufanya ili kufika kileleni kirahisi


Fahamu kuhusu mwili wako na akili


Ili kufahamu kuhusu mwili wako na sehemu gani una hisia zaidi unaweza kutumia vidole vyako na kuiweka akili yako ifikirie kuhusu ngono, jishike kwenye maeneo ambayo unahisi kuwa yanahisia nyingi kwa mikono na vidole vyako viwili, hisia zako zikiwa nyingi kwenye uke tumia vidole viwili kujisugua taratibu kwenye kinembe kwa kuzungusha vidole mbadala wa kuingiza ndani na nje kama uume unavyoingia na kutoka kwenye uke au tumia vifaa maalumu vinavyofanya kazi kama uume vilivyotengenezwa mahususi kuweza kukufikisha kileleni. Hii itakusaidia kujitambua ni kwa namna gani na muda gani ushiriki ili ufike kileleni. Baada ya hapo hamisha ulichojifunza kwa mpenzi wako kwa kumshirikisha ni namna gani afanye au kuchezesha uume wako ndani ya uke wako ili ufike kirahisi.


Unamshirikishaje mpenzi wako kuhusu maeneo ambayo una hisia zaidi?


Mara unapotambua kwamba maeneo furahi mwilini mwako yana hisia kali, mshirikishe mpenzi wako kwa ustaarabu na kwa vitendo. Mfano endapo unapata hisia zaidi ukishikwa kwenye kisimi kwa vidole, wakati wa ngono mshike mikono yake na iweke kwenye kisimi na jaribu kuchezesha vidole vyake vile unahisi unahisi raha, epuka kutoelewana kwa kumwambia ukinishika huko sipati hisia zozote nishike hapa. Pia mfano mwingine ni endapo unataka akunyonye shingo unaweza mwambia ukininyonyaga shingo Napata raha sana naye atakunyonya kiroho safi bila kuondoka kwenye mood yake.


Badili pozi na kutumia pozi la kuwa juu ya mpenzi wako.


Wanawake wengi hufika kirahisi endapo wanajishughulisha haswa pale wakiwa juu ya mwanaume badala ya mwanaume kuwa juu yao. Hii ni kwa sababu inakupa uwezo mkubwa wa kucheza juu ya uume, kwa kusugua uke ulio ndani ya uume. Hii itaruhusu uguse zaidi maeneo ambayo unahisia nyingi zaidi, endapo una hisia kwenye kisimi basi waza kuhusu kisimi chako kinavyogusa uume na furahisia hisia za kusugua uume kwenye kisimi chako. Endapo pozi hili halikupi raha au kufika kileleni tumia kifaa maalumu cha kusisimua kisimi ili kukusaidia kufika kileleni. Umuhimu wa pozi hili pia ni kwamba humfanya mwanaume achelewe kufika zaidi akilala juu yako na hii itakupa muda wewe kupata hisia ya uume mgumu ndani ya uke wako.


Namna kufanya ngono kwenye pozi hili


Unapokuwa juu ya mwanaume unaweza kulala pozi mbalimbali ili mradi usiumie kwenye shingo ya kizazi kwa uume kugusa huko, pozi la kulala na ambalo halitakusabaibishia kupata majeraha kwenye shingo ya kizazi na kufanya uguswe na uume kwenye G spoti ni kulala juu ya mwanaume kama inavyoonekana kwenye picha kushoto. Mpenzi wako anaweza kukupika kofi matakoni kwa kutumia nguvu kidogo. Kumbuka usilale ifudifudi bali jishikilie kwa kutumia viganja vya mikono yako kama inavyoonekana kwenye picha.


Zuia orgasm isiishe


Hii inasaidia kupata orgasm mara nyingi zaidi, madhumuni ni kusababisha presha ya orgasm iwe kali zaidi kabla ya kuachia iishe, mara unapokaribia hisia za raha kali, jizuie kufika orgasm kwa kuacha kufanya ngono kwa sekunde chache au kuwaza kitu kingie au unaweza tumia muda huu kubadili pozi ngono. Kufanya hivi kutakufanya ufike kirahisi na kupata raha kali zaidi.


Usifikirie kuhusu orgasm


Njia nzuri ya kufika kileleni haraka ni kuacha kufikiria kuhusu kufika kileleni, unaweza ukawa unafikiria kuhusu mazingira ya ndani ya chumba chako au kufanya mazungumzo wakati wa tendo au kufikiria kuhusu jinsi unavyovuta pumzi na kuitoa. Usifikirie kuhusu vitu ambavyo vinakuumiza kwa sababu utaondoka kwenye mood na uke wako utakauka.


Maeneo gani yakiguswa unaweza kupata orgasm?


Maeneo yafuatayo yakiguswa au kusisimuliwa yanaweza kusababisha upate orgasm kirahisi. Kumbuka unaweza kusisimuliwa maeneo mawili kwa pamoja na kuongeza uwezekano mkubwa wa kupata orgasm. Mfano ukiwa unasisimuliwa kwenye kisimi na wakati huo mpenzi wako akigusa maeneo yanayozunguka mlango wa haja kubwa unauwezekano wa kupata orgasm haraka zaidi.


Maeneo hayo ni;

 • Kisimi

 • Kuta za tundu la uke

 • Maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa. Hii ndio maana wakati wa orgasm misuli ya maeneo haya na njia husinyaa

 • Uke na kisimi kwa pamoja- maeneo haya yakisisimuliwa kwa pamoja huleta uwezekano wa kupata utamu mkali zaidi wa orgasm. Jifunze namna ya kusisimuliwa katika G spot yako

 • Maeneo mengine- baadhi ya wanawake hupata orgasm wakisisimuliwa maeneo mengine kama kuchezewa na kunyonywa chuchu kwa ulimi, kunyonywa masikio, shingo, bega au magoti. Endapo unahisia kali maeneo haya, yakinnyonywa au kuchezewa kwa muda mrefu huweza kupelekea kufika kileleni.


Je, kuna dawa za kuweza kukufikisha kileleni kirahisi?


Kuna dawa ambazo zimeruhusiwa na shirika la dawa kutumika kuwasaidia wanawake ambao hawapati hamu ya ngono kuwez akupata hamu, dawa yenye jina la Flibanserin na jina la kibiashara Addyi hutumika kwa wanawake walio na hamu kidogo au wasio na hamu kabisa ya kushiriki ngono. Dawa zingine pia za asilia zipo ambazo mwanamke anaweza kutumia ili kumsaidia kufika kileleni.


Kabla ya kutumia dawa ni vema ukafahamu kuwa, matibabu ya kutofika kileleni hutegemea kisababishi, endapo umetumia njia zote za hapo juu na bado hufiki kileleni basi ni vema kuwasiliana na daktari wako kwa uchunguzi wa kutambua tatizo lako na kupatiwa matibabu.


Wakati gani umwone daktari?


Endapo hujawahi kupata orgasm kabisa na licha kufuata ushauri huu, wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi wa hali au matatizo mbalimbali ya kiafya yanayoweza kupelekea kutofika kileleni. Baada ya visababishi vimezungumziwa kwenye makala zingine ndani ya tovuti hii, bonyeza hapa kusoma


Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa elimu na ushauri zaidi kwa kubonyeza “Pata tiba” au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.


Rejea za mada hii


 1. Uptodate. Treatment of female orgasmic disorder. https://www.uptodate.com/contents/treatment-of-female-orgasmic-disorder

 2. NIHS. https://www.nhs.uk/common-health-questions/sexual-health/what-is-an-orgasm/. Imechukuliwa 21.11.2020

 3. Healthline types of orgasm. https://www.healthline.com/health/healthy-sex/types-of-orgasms#the-stages-of-anorgasm. Imechukuliwa 21.11.2020

 4. Net doctor. Positions to make female orgasm easier during intercourse. https://www.netdoctor.co.uk/healthy-living/sex-life/a2283/positions-to-make-female-orgasm-easier-during-intercourse/. Imechukuliwa 21.11.2020

 5. ULY CLINIC. Matibabu ya Anorgasm. https://www.ulyclinic.com/anorgasm-kutofika-kileleni. Imechukuliwa 21.11.2020

 6. Webmd. FDA Approves First Drug to Boost Women’s Sex Drive. https://www.webmd.com/women/news/20150818/fda-approves-addyi-drug-boost-womens-sex-drive#1. Imechukuliwa 21.11.2020

 7. ULY CLINIC. Flibanserin. https://www.ulyclinic.com/dawa/Dawa-Flibanserin. Imechukuliwa 16/09/2021

3,584 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page