top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

Kutofika kileleni

Kutokufa kileleni kwa mwanamke -Anogazmia

Anogazmia ni neno la kitiba linalomaanisha kupata shida mara kwa mara kufika kileleni baada ya kusisimuliwa vya kutosha na ngono ama tendo la ndoa hivyo kupelekea dhiki binafsi. Anogazmia hutokea sana na huathiri wanawake zaidi kuliko unavyoweza kufikiria.

Kufika kileleni  hutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine kwa idadi ya mara ngapi kufika  kileleni na kiasi gani kinachohitajika kusisimuliwa ili kufika kileleni. 

 

Tafiti zinaonyesha wanawake chini ya theluthi moja  hufikia kileleni  mara kwa mara wakati wa kujamiana.  Tendo la kufikia kileleni  mara nyingi huathiriwa  umri, masuala ya matibabu au dawa unazotumia.

Kama wewe unafuraha na unafikia kileleni unapo jamiana, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Hata hivyo, kama wewe  unakelwa na tatizo la kutofika kileleni au kutofikia kileleni kama ulivyotarajia basi ongea na dakitari wako kuhusu tatizo hili akusaidie.

 

Ushauri kuhusu mabadiliko ya maisha na tiba  huweza kusaidia tatizo hili kupungua au kuisha.

ULY Clinic inakukumbusha kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yale yanayohusu afya yako.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kwa kupiga namba za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

Endelea kusoma kuhusu, Maana, Dalili, Visababishi, Matibabu kwa kuingia na email yako

bottom of page