top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

​

Dawa sindromu ya utumbo mfupi (Short bowel sindrome)

 

Sindromu ya utumbo mfupi hutokana na mgonjwa kufanyiwa upasuaji wa kukata sehemu kubwa ya utumbo kama tibaya magonjwa au saratani aina fulani. Wagonjwa hawa huhitaji matumizi ya dawa ili kuhakikisha kuwa kiasi cha kutosha cha chakula na maji kinafyonzwa na kuingia ndani ya mwili. Ufyonzaji wa dawa pia kwa watu wenye sindromu hii pia huathiriwa.

 

Madhumuni ya matibabu

 

Madhumuni ya matibabu haya ni kuhakikishakuwa  mgonjwa anapata kiasi cha kutosha cha dawa na lishe na kupunguza madhara kutokana na hali hii ya mgonjwa.

 

Matibabu ya dawa

 

Kwa wagonjwa wenye upungufu wa viinirishe

​

Huhitaji kupata vidonde vya kurejesha kiwango cha baadhi ya virutubisho ikitegemea sehemu ya utumbo iliyokatwa na kuondolewa. Wagonjwa hupata upungufu wa vitamin zifuatazo;

​

 

Mbali na upungufu wa vitamin wagonjwa hupata tatizo la haipomangnezimia ambapo madini ya magneziamu hupungua mwilini

 

Kuharisha sana

 

Wagonjwa wenye sindromu ya utumbo mfupi huharisha sana na hivyo hupoteza maji na madini. Wagonjwa hawa wanahitaji kutumia ORS kwa ajili ya kurejeza kiwango cha maji na madini yayayopotea kupitia kinyesi. Mgonjwa akipunguza kula chakula atapunguza kiwango cha kuharisha, hata hivyo hii italeta shida ya mgonjwa kupata upungufu wa lishe na utapiamlo. Mgonjwa anaweza kuhitaji kupewa chakula kwa njia ya mishipa kama imetokea ana harisha sana kusikokubalika.

​

Matibabu dawa yanaweza kuwa ya lazima pia. Uchaguzi wa dawa utategemea madhara yake na ukubwa wa sehemu ya utumbo iliyotolewa.

 

Dawa za kupunguza mijongeo ya matumbo

 

  • Loperamide hydrochloride

  • Codeine phosphate

  • Co-phenotrope

  • Colestyramine- kwa wagonjwa waliokatwa chini ya sentimita 100 za utumbo mwembamba(iliamu) ni muhimu kuangalia ugonjwa wa steatorea na upungufu wa vitamamini zinazochanganyika na mafuta

 

Dawa za kupunguza uzazlishaji wa vimeng’enya mwilini

 

  • Omeprazole- kwa wagonjwa wanaoharisha kutokana na kufanyiwa jujunostomi

  • Octreotide- kuharisha kutokana na kufanyiwa iliostomi

 

Fakta za ukuaji

 

Huweza kusaidia kuongeza uwezo wa tumbo kuhimili hali ya tatizo la sindromu ya utumbo mfupi mara baad aya upasuaji, hivyo kuimarisha ufyonzaji wa elekrolaiti, viinirishe na maji

Dawa hizo ni

  • Teduglutide- hufanana na glucagon like peptide 2

 

Ufyonzaji wa dawa

 

Dawa za kusafisha tumbo

  • Citric acid yenye magneziamu carbonate

  • Macrogol 3350 yenye anhydrous sodium sulfate, ascorbic acid, potassium chloride, sodium ascorbate na sodium chloride

  • Magnesium citrate yenye sodium picosulfate

bottom of page