top of page

Imeandikwa na Daktari wa ulyclinic

​

Ulimi wa  jiografia

 

Utangulizi

​

Ulimi wa jiografia au ulimi ramani kwa lugha ya kiingereza "geographic tongue" hutokana na ni michomo ya kinga za mwili ambayo huathiri sakafu ya juu au kwenye pembe za kushoto na kulia ya ulimi. Tatizo hili halina madhara yoyote kwa binadamu. Tafiti nyingi zimeonesha ulimi jiografia huambatana na matatizo ya pumu ya Ngozi, licheni planas na soriasisi

 

Tatizo hili husababisha ulimi uonekane kuwa umefunikwa na mabaka madogo meupe au ya kuchanganyika na rangi ya pinki pamoja na na vipele vidogo ambavyo  ni tezi za radha za papilla.

​

Hata hivyo mabaka hayo mara nyingi huwa hayana tezi za papilla na huonekana kama kisiwa chenye eneo laini jekundu na kingo zake huwa na mwinuko mdogo , unaofanya  ulimu kuwa na mwonekano wa ramani.

 

Mabaka haya huwa na tabia ya kuhama sehemu moja kwenda nyingine mara baada ya ulimi kupona.

​

Ingawa tatizo hili linaogopesha kutokana na ubadilika kwa mwonekano wa ulimi, tafiti zinaonyesha tatizo hili kutoambatana na shida yoyote mwilini ikiwa pamoja na maambukizi au saratani.

 

Mambo ambayo yanaweza kuhusiana na ulimi jiografia ni pamoja na kuhisi vitu hivi vimezidi kama vile vitu vitamu, viungo, na hata chumvi.

 

​

Endapo umepatwa na tatizo hili unaweza kuwasilianana daktari wako kwa ushauri na vipimo zaidi

​

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri na matibabu sasa kwa kubonyeza hapa au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii

 

Kundelea kusoma kuhusu kwa kubonyeza unachotaka, itakuhitaji utumie email yako tu

​

​

ulimi ramani-ulyclinic
Utangulizi
bottom of page