top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 08:44:23
Eti ZAHA-500 inatibu ugonjwa gani??
Zaha ni jina la kibiashara la dawa azithromycin. Inatibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria, ikiwa ni pamoja na:
**- Maambukizi makali kwenye mapafu
- Sinusaitisi kali
- Nimonia ya jamii
- Maambukizi ya wastani kwenye ngozi
- Maambukizi kwenye urethra na shingo ya kizazi
- Vidonda sehemu za siri
- Maambukizi makali kwenye sikio
- Falinjaitisi/Tonsilaitisi(maambukizi kooni na kwenye tezi tonsesi)**
Ni vyema kuwasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
8 Septemba 2026, 01:00:01
bottom of page

