top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 12:51:08

Je magego ya mtoto yakiwa yanatoka meno yanaweza kupasuka?

Jino lolote linaweza kupata ufa au kuvunjika katika kipindi chochote bila kuhusuana na kipindi ambacho mtoto anaota meno ya nyuma, hivyo gego linalochomoza halisababishi moja kwa moja jino jingine kupasuka.


Kama jino lingine limepasuka wakati huo, sababu inaweza kuwa:

  • Jino hilo tayari lilikuwa dhaifu au lina tundu.
  • Mtoto ameuma kitu kigumu.
  • Kuna msuguano au nguvu kubwa ya kutafuna.
  • Jino lina kasoro ya enamel iliyokuwepo tangu lilipokuwa linatengenezwa.
  • Kama ni jino la maziwa, wakati mwingine linaweza kuwa limeathiriwa na kuoza na hivyo kuvunjika kirahisi.

Kwa hiyo, kuota kwa molars na kupasuka kwa jino jingine kunaweza kutokea kwa wakati mmoja, lakini hakuna uhusiano wa moja kwa moja kwamba molar inayotoka ndiyo imelipasua jino lingine.


Ikiwa ufa unaonekana kwenye jino la mtoto, hasa kama jino limeanza kubadilika rangi, kuuma, kuvimba au kipande kimevunjika, ni vizuri daktari wa meno aliangalie ili kujua kama ni ufa halisi, tundu au umbo la kawaida la jino.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

1 Septemba 2026, 14:17:14

​

bottom of page