top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Je ukimeza dawa hiyo misoprostol ndani ya siku 3 unahalisha ujaona damu je hiyo ni dalili nzuri au mbaya?

Kama umetumia misoprostol kwa ajili ya kutoa ujauzito na baada ya siku 3 hujaona damu kabisa, hiyo si dalili nzuri ya kuthibitisha kwamba dawa imefanya kazi. Kitaalamu, kutokutokwa damu baada ya misoprostol kunaweza kuashiria kuwa ujauzito haujatoka au dawa haikufanya kazi ipasavyo; pia, ingawa si kawaida, kuna uwezekano wa ujauzito wa nje ya kizazi ambao misoprostol haiwezi kuitoa.


Kwa kawaida damu na maumivu huanza ndani ya saa kadhaa baada ya misoprostol, ingawa muda unaweza kutofautiana. Kutokutokwa damu kabisa ndani ya saa 24 kunapaswa kufuatiliwa na mhudumu wa afya.


Kwa hiyo baada ya siku 3 bila damu, ni muhimu kupimwa/kuwasiliana na mhudumu wa afya ili kuthibitisha kama ujauzito bado upo na kuondoa uwezekano wa ectopic pregnancy. Usiongeze dozi nyingine kwa kubahatisha bila kujua umri wa ujauzito na regimen uliyotumia.


Nenda hospitali haraka ikiwa una maumivu makali au yanayoongezeka upande mmoja wa tumbo, kizunguzungu/kuzimia, maumivu ya bega, au udhaifu mkubwa hizi zinaweza kuwa dalili za ujauzito wa nje ya kizazi au tatizo jingine linalohitaji matibabu ya haraka.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

23 Septemba 2026, 12:43:10

​

bottom of page