top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Je, vipele vigumu sehemu za siri ni dalili ya nini?? na vina sababishwa na nini??

Vipele vigumu sehemu za siri vinaweza kusababishwa na hali mbalimbali, zikiwemo:


  • Sunzua sehemu za siri (HPV): huwa vipele vilivyoinuka, vya rangi ya ngozi na vinaweza kuwa laini au kuwa na uso usio sawa. Husababishwa na baadhi ya aina za HPV na huweza kuongezeka au kuungana.
  • Vipele Fordyce ni tezi za mafuta zinazoonekana kama vijipele vidogo vyeupe au vya njano. Si ugonjwa wa zinaa na haviambukizi.
  • VIpele lulu (Pearly penile papules): kwa mwanaume, huwa vijipele vidogo vya rangi ya ngozi vinavyopangwa kwa mstari kuzunguka kichwa cha uume. Ni hali ya kawaida ya mwili na si maambukizi ya zinaa.
  • Vipele vya Molluscum contagiosum: husababisha vijipele vidogo, vigumu na vinavyong'aa, mara nyingi vikiwa na shimo dogo katikati. Kwa watu wazima vinaweza kuenea kupitia mawasiliano ya ngono.
  • Maambukizi kwenye shina la nywele au nywele kuotea ndani: inaweza kutokea hasa kwenye maeneo yenye nywele, kwa mfano baada ya kunyoa.
  • Vipele vya Kaswende: katika hatua ya awali inaweza kusababisha kidonda au uvimbe mgumu usio na maumivu sehemu ya siri, hivyo si kila uvimbe mgumu una maana ya HPV.

Kwa hiyo, “vipele vigumu” pekee hazitoshi kutambua ugonjwa. Daktari anaweza kuhitaji kuangalia ukubwa, rangi, mpangilio, eneo, kama vinauma au kuwasha na kama vinaongezeka. Baadhi ya vipele vinaweza kutambuliwa kwa kuangalia tu, lakini wakati mwingine vipimo au biopsy huhitajika.


Kama vipele ni vipya, vinaongezeka, vinatoa damu, vina vidonda, vinauma, au vilianza baada ya kufanya ngono bila kinga, ni vizuri kupimwa kwenye kliniki ya ngozi au magonjwa ya zinaa badala ya kutumia dawa bila kujua chanzo.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

8 Septemba 2026, 01:27:37

​

bottom of page