top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

10 Oktoba 2026, 09:38:37

Kichwa kinauma mara kwa mara

Kichwa kuuma mara kwa mara kunaweza kusababishwa na hali mbalimbali, kama vile:


  • Kipandauso: Huleta maumivu ya wastani hadi makali, wakati mwingine yakifuatana na kichefuchefu na kutovumilia mwanga au sauti.
  • Maumivu ya kichwa ya mkazo: Huenda yakahusiana na msongo wa mawazo, kukosa usingizi au misuli ya shingo kukaza.
  • Upungufu wa maji mwilini: Kutokunywa maji ya kutosha kunaweza kuchangia maumivu ya kichwa.
  • Matatizo ya macho: Hitaji la miwani au matatizo mengine ya kuona yanaweza kuchangia maumivu.
  • Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za maumivu: Kutumia baadhi ya dawa za maumivu mara nyingi kunaweza kufanya kichwa kiendelee kuuma.

Ufanye nini?

  • Kunywa maji ya kutosha, lala kwa muda wa kutosha na kula kwa ratiba inayofaa.
  • Andika muda maumivu yanapoanza, yanapodumu na vitu vinavyoonekana kuyachochea.
  • Ikiwa kichwa kinauma mara kwa mara, panga uchunguzi wa daktari ili kubaini chanzo badala ya kuendelea kutumia dawa za maumivu bila tathmini.

Nenda hospitalini mara moja ikiwa maumivu yanaanza ghafla na kuwa makali sana, au yanaambatana na udhaifu wa mwili, ganzi, kuchanganyikiwa, kuona kwa shida, homa pamoja na shingo kukakamaa, au kutapika kusikokoma.


Muhimu: Presha kuwa kawaida hakumaanishi kwamba sababu zote za maumivu ya kichwa zimeondolewa. Uchunguzi hutegemea aina ya maumivu, muda wake na dalili zinazoambatana nayo.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

9 Oktoba 2026, 11:29:03

​

bottom of page