top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 12:15:51

Kipimo Cha 4th generation ya antibody/Antigen COMB kina fanyika baada ya muda gani ukishamaliza PEP?

Kwa mtu aliyemaliza PEP ya siku 28:


  • Kipimo cha Kizazi cha 4 cha Ag/Ab kinaweza kufanyika takribani wiki 4–6 baada ya kuanza PEP kama kipimo cha ufuatiliaji, lakini majibu hasi wakati huu hayatoi uhakika wa mwisho kwa sababu PEP inaweza kuchelewesha kugundulika kwa maambukizi.
  • Kwa kipimo cha mwisho, miongozo ya sasa inapendekeza Kipimo cha kizazi cha 4 Ag/Ab pamoja na HIV NAT takribani wiki 12 baada ya kuanza PEP, sawa na karibu wiki 8 baada ya kumaliza PEP.
  • Shirika la Afya Duniani pia inapendekeza ufuatiliaji wa Maambukizi ya VVU baada ya PEP, huku kipimo cha karibu miezi 3 baada ya tukio la hatari kikitumika katika ufuatiliaji.

Mfano: Ikiwa PEP ilimalizika baada ya siku 28, kipimo cha mwisho kinachofanywa karibu wiki 8 baada ya kumaliza PEP ni muhimu zaidi kuliko kutegemea kipimo cha mapema pekee.


Ikiwa kuna uwezekano wa tukio jingine la hatari baada ya lile la awali, muda wa ufuatiliaji unapaswa kuhesabiwa kwa kuzingatia tukio hilo pia.


Kwa hiyo, usiichukulie Hasi ya kizazi cha 4 iliyofanyika mapema sana baada ya PEP kama jibu la mwisho bila kuzingatia muda na ushauri wa mtoa huduma.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

2 Septemba 2026, 11:30:05

​

bottom of page