Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
30 Septemba 2026, 14:47:19

Matumizi ya foliki asidi yakoje kwa mtu aliyeanza kutumia akiwa na mimba ya miezi minne?
Mtu aliyeanza kutumia foliki asidi akiwa na ujauzito wa miezi minne bado anashauriwa kuendelea kuitumia kulingana na maelekezo ya mtoa huduma wa afya. Ingawa faida yake katika kuzuia kasoro za ubongo na uti wa mgongo wa mtoto huwa kubwa zaidi inapotumiwa kabla ya mimba na katika wiki za mwanzo za ujauzito, kuanza baada ya muda huo hakumaanishi kwamba foliki asidi haina umuhimu tena.
Kwa mara nyingi madaktari wanaweza hushauri;
- Dozi ya kawaida: Mikrogrumu 400 (miligramu 0.4) kwa siku, isipokuwa kama umepewa dozi tofauti na mtoa huduma wa afya.
- Ikiwa unatumia madini chuma pamoja na foliki asidi: Endelea kutumia kulingana na maelekezo ya kliniki, kwa sababu virutubisho vya chuma na foliki asidi hupendekezwa wakati wa ujauzito.
- Usitumie dozi kubwa bila ushauri: Foliki asidi ya miligramu 5 kwa siku hutolewa kwa baadhi ya wanawake walio katika hatari maalumu na si dozi ya kutumia bila maelekezo.
- Usiache huduma ya kliniki: Miezi minne ya ujauzito bado ni muhimu kwa kufuatilia ukuaji wa mtoto, lishe ya mama na virutubisho vingine vinavyohitajika.
Kwa hiyo, kuanza foliki asidi katika mwezi wa nne si sababu ya kuogopa wala kuacha kuitumia. Endelea kuitumia kwa dozi uliyoelekezwa na mtoa huduma wako wa afya na kuhakikisha unaendelea na kliniki ya ujauzito.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
22 Agosti 2026, 18:56:59

