Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD,
Mhariri:
Dkt. James NL, MD
Imeboreshwa:
26 Septemba 2026, 12:29:08
Nataka kujua mazala ya Prednisolone
Prednisolone ni dawa ya kundi la kotikosteroidi. Hutumika kupunguza uvimbe na mwitikio wa kinga mwilini, kwa mfano katika baadhi ya magonjwa ya mzio, pumu, magonjwa ya ngozi, viungo na magonjwa mengine ya uchochezi kinga.
Madhara yanayoweza kutokea hutegemea dozi na muda wa kutumia dawa, na yanaweza kujumuisha:
- Kuongezeka kwa hamu ya kula
- Kuongezeka uzito
- Kuongezeka kwa sukari kwenye damu
- Kuongezeka kwa shinikizo la damu
- Kukosa usingizi au kubadilika kwa hisia
- Kiungulia au usumbufu wa tumbo
- Kuongezeka kwa hatari ya kupata maambukizi
- Kwa matumizi ya muda mrefu: ngozi kuwa nyembamba, mifupa kudhoofika, matatizo ya macho na mwili kupunguza uzalishaji wake wa kawaida wa kotokosteroidi.
Muhimu: Prednisolone haipaswi kuachwa ghafla ikiwa imetumika kwa muda mrefu au kwa dozi kubwa; daktari anaweza kuhitaji kupunguza dozi taratibu.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeandikwa,
1 Septemba 2026, 23:43:10

