top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 08:44:23

Natokwa na uchafu wa rangi ni kama usaha ikiambatana na miwasho, shida ni nini?

Uchafu unaofanana na usaha pamoja na muwasho kwenye sehemu za siri unaweza kutokea kwa mwanaume au mwanamke na mara nyingi huhitaji uchunguzi ili kujua chanzo.


  • Kwa mwanaume: uchafu unaotoka kwenye tundu la uume pamoja na muwasho au kuwaka wakati wa kukojoa unaweza kuhusishwa na kisonono, klamidia, au maambukizi mengine ya njia ya mkojo au magonjwa ya zinaa.
  • Kwa mwanamke: uchafu mzito au unaofanana na usaha pamoja na muwasho unaweza kuhusishwa na maambukizi ya uke, kisonono, klamidia, trichomoniasis au maambukizi mengine, kulingana na rangi, harufu na dalili zinazoambatana nao.

Kwa kuwa dalili hizi zinaweza kusababishwa na maambukizi tofauti, ni vizuri kupimwa badala ya kuanza dawa bila kujua chanzo. Vipimo vinaweza kujumuisha sampuli ya uchafu au kipimo cha mkojo kwa kisonono na klamidia, pamoja na vipimo vingine vya magonjwa ya zinaa kulingana na dalili na historia ya tendo la ngono.


Ni vyema kuepuka ngono mpaka uchunguzi ufanyike na, ikiwa maambukizi yatathibitika, mwenye maambukizi pamoja na mwenza wake watibiwe ipasavyo.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

8 Septemba 2026, 00:53:42

​

bottom of page