top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD,

Mhariri:

Dkt. James NL, MD

Imeboreshwa:

26 Septemba 2026, 10:56:46

Yapi ni magonjwa ya zinaa?

Magonjwa ya zinaa ni maambukizi yanayoweza kuambukizwa kupitia ngono, ikiwemo ngono ya uke, njia ya haja kubwa au mdomo.


Miongoni mwa magonjwa ya zinaa ni:



1. Klamidia (Chlamydia)

**2. Kisonono (Gonorrhea)

**3. Trikomoniasisi (Trichomoniasis)

**4. Kaswende (Syphilis)

**5. Homa ya ini aina B (Hepataitisi B)

**6. Homa ya ini aina C (Hepataitisi C)

**7. Virusi vya herpes aina ya 1 na 2 (Herpes)

**8. Virusi vya UKIMWI (VVU)

**9. Kirusi cha human papilloma (HPV)

10. Pangusa (chankroidi)

11. Limfagranuloma veneramu (LGV)

12. Donovanosisi (granuloma inguinale)


Muhimu: Si kila ugonjwa unaoweza kuambukizwa wakati wa ngono ni “ugonjwa wa zinaa” kwa maana ya kawaida. Kwa mfano, baadhi ya maambukizi ya ngozi, fangasi au bakteria wa kawaida yanaweza kuhamishwa wakati wa tendo bila kuwa magonjwa y zinaa ya kawaida.


Pia, mtu anaweza kuwa na magonjwa ya zinaa bila dalili yoyote, hivyo kutokuwepo kwa dalili hakumaanishi hakuna maambukizi.


Soma zaidi kuhusu magonjwa ya zinaa, Bofya 👉Magonjwa ya zinaa.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeandikwa,

2 Septemba 2026, 18:23:37

​

bottom of page