Mwandishi:
Dkt. Charles W, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, M.D
Jumatano, 19 Julai 2023
Maudhi ya PEP
Maudhi ya PEP ni madhara madogo yanayotokana na matumizi ya PEP. Mara nyingi unavuoanza kutumia PEP utaanza kuhisi na kuona mabadiliko mbalimbali mwilini mwako ambayo yataisha kwa jinsi siku zinavyoenda.
Maudhi ya PEP ni yapi?
Maudhi ya PEP yanayotokea hutegemea aina ya dawa inayotumika, katika sehemu hii utajifunza maudhi yanayotokea sana na yale ya nadra kwa mchanganyiko wa dawa zinazotumika ambazo ni;
1. Tenofovir EMT na Dolutegravir au na raltegravir
Na mbadala wake ambao huwa na mchanganyiko
2. Tenofovir EMT na darunavir (DRV)(800 mg) au na ritonavir
Kumbuka: Tenofovir EMT ni mchanganyiko wa tenofovir na Emtricitabin)
Maudhi makuu ya Tenofovir EMT
Kichefuchefu
Mvurugiko wa tumbo
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu
Udhaifu
Uchavu mkali
Maudhi ya nadra ya Tenofovir EMT
Matatizo ya figo
Kusinyaa kwa mifupa
Maudhi haya hutokea kama ikitumika kwa muda mrefu.
Maudhi makuu ya Dolutegravir
Kichefuchefu
Maumivu ya kichwa
Kuhara
Maudhi ya nadra ya Dolutegravir
Matatizo ya figo
Harara
Mzio wa dawa
Maudhi ya Darunavir
Maumivu ya kichwa
Kuhara
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Haja ngumu
Maudi ya ritonavir
Usingizi mzito
Kuhara
Gesi tumboni
Kiungulia
Kubadilika kwa uwezo wa kutambua ladha
Maumivu ya kichwa
Gamzi, hisia za kuungua, kuchomachoma kwenye viganja vya mikono, miguu na midomo
Maumivu ya misuli au maungio ya mifupa
Kicefuchefu
Kutapika
Kwa ujumla maudhi yanayotokea hutegemea mchanganyiko wa dawa unazotumia, ili kufahamu zaidi kuhusu maudhi ya dawa ulizopewa, angalia maudhi katika kila dawa unayotumia.
Dalili kali za matumizi ya PEP
Kama ukipata dalili kali za matumizi ya PEP onana na daktari haraka iwezekanavyo. Miongoni mwa dalili hizo ni;
Harara kwenye ngozi
Kubabuka au kuungua ngozi
Vidonda kwenye midomo
Macho kuwa mekundi, kuvimba, kuwasha au kutokwa machozi
Maumivu ya misuli maungio ya mifupa
Homa
Kuvimba, maumivu au dalili za maambukizi
Kichefuchefu kikali
Uchovu mkali
Kukosa hamu ya kula
Maumivu upande wa kulia juu ya tumbo chini ya mbavu
Kinyesi kuwa cheusi au kilichopauka
Manjano machoni au kwenye ngozi
Kizunguzungu
Mapigo ya moyo kwenda tofauti na kawaida
Kizunguzungu
Kuoteza fahamu
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?
Unaweza kupata maelezo zaidi kwa kubofya katika makala zifuatazo:
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Agosti 2024 18:41:58
Rejea za mada hii:
1. ULY CLINIC. Madhara ya kutumia PEP kwa muda mrefu. https://www.ulyclinic.com/majibu-ya-maswali/je-kuna-madhara-yoyote-ya-kutumia-pep-kwa-muda-mrefu%3F. Imechukuliwa 19.07.2023
2. The Alfred. PEP Information. https://www.alfredhealth.org.au/images/resources/patient-resources/PEP-Information.pdf. Imechukuliwa 19.07.2023
3. NCBI. Tenofovir. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK548917/#:. Imechukuliwa 19.07.2023
4. Cada DJ, et al. Dolutegravir. Hosp Pharm. 2014 Feb;49(2):184-95. doi: 10.1310/hpj4902-184. PMID: 24623872; PMCID: PMC3940684.
5. ULY CLINIC. Dolutegravir. https://www.ulyclinic.com/dawa/Dolutegravir. Imechukuliwa 19.07.2023
6. ULY CLINIC Tenofovir.https://www.ulyclinic.com/dawa/Tenofovir.Imechukuliwa 19.07.2023
7. Medline plus. Darunavir. https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a607042.html. Imechukuliwa 23.07.2023
8. Medlineplus. Ritonavir. https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a696029.html.Imechukuliwa 23.07.2023
9. CDC. PEP. https://www.cdc.gov/hiv/clinicians/prevention/prescribe-pep.html. Imechukuliwa 23.07.2023