top of page

Vidokezo vya Afya

Mtindio wa ubongo

Mtindio wa ubongo

Mtindio wa ubongo kwa mtoto unaweza kusababishwa na hali au magonjwa yanayozuilika na kutibika kama homa ya uti wa mgongo, homa ya ubongo, malaria ya ubongo na majeraha kichwani. Muwahishe mwanao kwa tiba anapopata dalili za magonjwa haya.

Mtoto akiwa na homa

Mtoto akiwa na homa

Mtoto akiwa na homa ya nyuzi joto za selsiasi 38 au zaidi kwa siku tatu mfululizo, isiyoshuka kwa dawa, au kupata dalili za hatari kama degedege, harara kwenye ngozi, kukakamaa shingo, maumivu ya kichwa, kuharisha, vidonda kooni, maumivu ya sikio, kukataa kula au kunywa, kuwa dhaifu au kutapika. Wasiliana na daktari mara moja.

Mtoto kuacha kupumua kwa zaidi ya sekunde 20

Mtoto kuacha kupumua kwa zaidi ya sekunde 20

Mtoto kuacha kupumua kwa zaidi ya sekunde 20 siku ya kwanza ya kuzaliwa ni kiashiria cha tatizo la kiafya kwa mtoto. Muwahishe hospitali kwa tiba.

Mtoto kuvuta maji yaliyo changanyika na kinyesi

Mtoto kuvuta maji yaliyo changanyika na kinyesi

Mtoto kuvuta maji yaliyo changanyika na kinyesi chache cha kwanza wakati wa kuzaliwa ni kisababishi cha matatizo ya upumuaji kwa mtoto.

Mtoto njiti hupatwa na magonjwa

Mtoto njiti hupatwa na magonjwa

Mtoto njiti au aliyezaliwa na uzito chini ya kilo 2.5 ni kihatarishi cha kushambuliwa na magonjwa ya utotoni. Fuata ushauri wa daktari mkinge mwanao.

bottom of page