top of page

Imeandaliwa namadaktari wa ULY-Clinic

 

 

Vimbe ndani ya mfuko wa uzazi; Uterine Fibroids

 

Fibroids ni Vimbe zisizokuwa na sifa ya saratani, hazibadiliki kuwa saratani zinapotokea kwa mwanamke na  si kihatarishi cha kupata saratani katika mfuko wa uzazi.

 

Vimbe hizi huanza kipindi cha uzazi yaani kipindi mwanamke anauwezo wa kubeba mimba na hutokea sana kati ya umri wa miaka 35- 45. Fibroids au kwa jina jingine ni leiomyoma hukua sehemu mbalimbali za misuli ya mfuko wa uzazi kama, katikati ya misuli ya ukuta wa kizazi au ndani,. Ukuaji wa vimbe hizi huwa wa tofauti sana kati ya mtu na mtu au kati ya uvimbe na uvimbe kwa mtu mmoja.

 

Vimbe zingine hukua haraka sana na zingine huweza kukua polepole au wakati mwingine kutokua kabisa. Baadhi ya vimbe hizi huweza kuwa kubwa zaidi ya mpira wa miguu kiasi cha  kufikia kwenye mbavu na kusababisha matatizo ndani ya tumbo na zingine huweza kuwa ni ndogo sana na kutonekani wala kutoa dalili yoyote na pia wakati mwingine vimbe hizi husinyaa na kupotea kabisa.

 

Hivyo wanawake wengi (wa 3 kati ya wa4 ) wana vimbe hizi lakini wengi wao hawatambuliki kwa sababu huwa haziwasababishii matatizo yoyote katika mfumo wa kizazi au tumboni na kwa bahati mbaya dakitari anaweza kuzitambua akiwa anafanya kipimo cha kuchunguza mwili na pia wakati wa kipimo cha mionzi ya sauti (ultrosound)

 

bottom of page