Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Sospeter B, MD
19 Septemba 2021 12:22:29
Kirusi mshirika wa Adeno
Kirusi mshirika wa Adeno ni kirusi chenye strendi moja ya DNA kinasababisha maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji na husambazwa kwa njia ya hewa. Kirusi huyu huambatana mar azote na kirusi adeno na na hufahamika pia kama Adeno associated virus.
Kirusi mshirika wa Adeno huenezwa mwaka gani?
Tafiti zinaonesha kirusi adeno associated kiligundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1950 kwenye tishu zilizo nyuma ya pua.
Kirusi mshirika wa Adeno kipo katika Familia gani?
Kirusi mshirika wa Adeno ni kimoja wapo kwenye genus ya Dependovirus na familia ya Parvoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi mbili ya DNA pia husababisha maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Sifa za kirusi
Kirusi mshirika wa Adeno ni moja ya kirusi chenye strendi moja ya DNA katika familia ya virusi vya Parvoviridae. Kirusi huyu huwa na sifa zifuatazo;
Ana DNA moja
Ana Strendi moja ya DNA
Ukuta wa nje ya seli haujafunikwa
Wana umbile lenye pande ishirini na kipenyo cha 18–26 nm
Jinomu yake ina wastani wa urefu wa kilobezi 4.8
Familia ya Kirusi mshirika wa Adeno
Parvoviridae imegawanyika katika familia mbili;
Parvovirinae
Densovirinae
Aina ya Kirusi mshirika wa Adeno
Kuna aina kumi na moja za kirusi mshirika wa Adeno ambazo ni;
Adeno associated serotype 1
Adeno associated serotype 2
Adeno associated serotype 3
Adeno associated serotype 4
Adeno associated serotype 5
Adeno associated serotype 6
Adeno associated serotype 7
Adeno associated serotype 8
Adeno associated serotype 9
Adeno associated serotype 10
Adeno associated serotype 11
Kirusi mshirika wa Adeno vinavyopatikana kwenye seli za binadamu ni pamoja na;
Kirusi mshirika wa Adeno serotaipe 2 (Adeno associated serotype 2)
Kirusi mshirika wa Adeno serotaipe 3 (Adeno associated serotype 3)
Kirusi mshirika wa Adeno serotaipe 5 (Adeno associated serotype 5)
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi mshirika wa Adeno hutunzwa na binadamu pamoja na wanyama wenye mti wa mgongo.
Kirusi mshirika wa Adeno kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi mshirika wa Adeno kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua
Wakati mwingine watu huambukizwa Kirusi mshirika wa Adeno wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni
Kukaa karibu na mtu mwenye maambukizi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya Kirusi mshirika wa Adeno
Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo ya Kirusi mshirika wa Adeno
Watoto chini ya miaka mitano
Wenye upungufu wa kinga mwilini
Dalili za Maambukizi ya Kirusi mshirika wa Adeno
Dalili za Maambukizi ya Kirusi mshirika wa Adeno ni;
Pua kutoa uchafu (makamasi)
Kupata homa
Kikohozi kikavu
Kichwa kuuma
Macho kubadirika rangi
Maambukizi kwenye mapafu
Koo kuuma
Vipimo vya Kirusi mshirika wa Adeno
RT-PCR
Kuotesha kirusi
Picha nzima ya damu
Kipimo cha seroloji
Kipimo cha antigen
Radiografia ya kifua
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na maambukizi ya Kirusi mshirika wa Adeno
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na maambukizi ya Kirusi mshirika wa Adeno ni pamoja na;
Bacterial pharyngitis
Bacterial pneumonia
Bronchitis
Nimonia ya kuambukizwa kwenye jamii
Coronavirus disease 2019
Influenza
Mycoplasmal pneumonia
Pertusis
Maambukizi katika mfumo wa juu wa njia ya hewa
Nimonia ya kirusi
Matibabu ya maambukizi ya Kirusi mshirika wa Adeno
Hakuna matibabu maalum kwa ajiri ya maambukizi ya kirusi cha Adeno associated ila mgonjwa anaweza pata yafuatayo;
Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa
Mgonjwa atapatiwa maji ya kutosha kwa njia ya mishipa au kunywa
Mgonjwa anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika
Mgonjwa atapata panadol kwa ajiri ya maumivu na homa
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi
Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu
Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye
Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka
Pata chanjo ya kirusi mshirika wa Adeno kwa wakati sahihi
Osha mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote
Je kuna chanjo ya Kirusi mshirika wa Adeno?
Chanjo kwa ajiri ya Kirusi mshirika wa Adeno ipo.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea zamada hii;
NCBI. Adeno associated virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5548848/. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
Sciencedirect. Adeno Associated Virus. https://www.sciencedirect.com/topics/immunology-and-microbiology/adeno-associated-virus. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
Sciencedirect. Adeno associated virus. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/adeno-associated-virus. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
CDC. Adeno associated virus. https://www.cdc.gov/adenovirus/about/symptoms.html. Imechukuliwa 15/09/2021.Â
Medscape. Adeno associated virus. https://emedicine.medscape.com/article/211738-overview. Imechukuliwa 15/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:10:43