top of page

Mwandishi;

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri;

Dkt. Benjamin L, MD

5 Oktoba 2021 17:04:37

Human respiratory syncytial virus

Human respiratory syncytial virus

Kirusi Human respiratory syncytial ni kirusi kinachosababisha maambukizi kwenye mfumo wa chini wa upumuaji hasa kwa watoto wadogo kabla hawajafikisha miaka miwili.


Kirusi husababisha nini?


Kirusi hiki husababisha maambukizi kwenye mfumo wa chini wa upumuaji


Kirusi kilianza mwaka gani?


Kirusi human respiratory syncytial kigundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1956 wakati mtafiti alitoona kirusi katika majimaji kutoka kwa sokwe mtu aliyekuwa na dalili za ugonjwa wa mapafu na hivyo kuitwa jina la Chimpanzee Coryza Agent. Mwaka 1957 kirusi alitambuliwa kwa mtoto mdogo na kikaonekana kusababisha maambukizi wka watoto wadogo kabla ya kufikisha miaka miwili na hivyo kikapewa jina la human orthopneumovirus au human respiratory syncytial virus


Kirusi Human respiratory syncytial kipo katika Familia gani?


Kirusi Human respiratory syncytial ni kimoja wapo kwenye genus ya Orthopneumovirus na familia ya Pneumoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha maambukizi katika mfumo wa upumuaji.


Sifa za kirusi


Human respiratory syncytial ni kirusi chenye strendi moja ya RNA hasi katika familia ya virusi vya Pneumoviridae yenye sifa zifuatazo;

 • Strendi moja ya RNA

 • Urefu wa 15-28kb

 • Wana RNA hasi

 • Ukuta wa seli yake umefugwa


Kirusi hutunzwa na nani?


Kirusi Human respiratory syncytial hutunzwa na binadamu.


Kirusi Human respiratory syncytial kinaenezwa kwa njia gani?


Kirusi Human respiratory syncytial kinaenezwa kwa njia zifuatazo;


Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua.

Wakati mwingine watu huambukizwa wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni.


Vihatarishi vya kupata maambukizi


 • Watoto wadogo wenye matatizo ya mapafu ya muda mrefu.

 • Mkusanyiko mkubwa wa watu

 • Mtu yeyote anayekaa karibu na mtu mwenye maambukizi.

 • Watu ambao kinga ya mwili imeshuka.

 • Watoto waliozaliwa kabla ya muda.

 • Watoto ambao hawajanyonya vizuri.

 • Watoto waliozaliwa zaidi ya wawili.

 • Uchafuzi wa mazingira.


Dalili za maambukizi ya kirusi Human Respiratory syncytial


Muda wa kuatema ni ndani ya siku tatu hadi tano. Mtu mwenye maambukizi ya kirusi respiratory syncytial huweza kumuambukiza mwingine hata kabla dalili hazijaonekana. Dalili za maambukizi ya kirusi respiratory syncytial;


 • Kikohozi

 • Homa

 • Kushindwa kupumua vizuri

 • Sayanosis

 • Mafua

 • Kuingia ndani kwa misuli ya kifua

 • Miruzi ya kifua

 • Sepsis

 • Rales


Vipimo


 • Picha nzima ya damu

 • Kuotesha kirusi

 • Polymerase chain reaction

 • Kipimo cha mkojo

 • Serum electrolyte concentration

 • Picha nzima ya kifua

 • Kipimo cha oxygen


Magonjwa yanayofanana


 • NImonia ya watoto

 • Bronkaitiz ya watoto

 • Sepsis kwa viachaga

 • Influenza

 • Bronnkolaitiz

 • Adenovirus

 • Croup

 • Human metapneumonia virus

 • Human parainfluenza virus


Matibabu


 • Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya homa na maumivu

 • Mgonjwa dawa aina ya bronchodilator

 • Mgonjwa atapatiwa maji mengi kwa njia ya mshipa au kunywa

 • Mgonjwa atapatiwa Ribavirin kama antiviral

 • Mgonjwa atapatiwa oxygen endapo oxygen yake itakuwa chini


Je kuna chanjo ya kirusi Human Respiratory syncytial?


Mpaka sasa hakuna chanjo ya kirusi respiratory syncytial.


Kinga


 • Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu

 • Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye

 • Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka

 • Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji safi na sabuni

 • Usiguse macho yako, pua na mdomo

 • Usikae karibu na mtu mwenye maambukizi

Imeboreshwa;

5 Oktoba 2021 17:31:41

bottom of page