top of page

Mwandishi;

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri;

Dkt. benjamin L, MD

27 Septemba 2021 07:01:33

Kirusi Hepatitis A

Kirusi Hepatitis A

Kirusi Hepatitis A ni aina kirusi anayesababisha homa ya ini inayoweza kuwa ya wastani au kali na inayoweza kudumu kwa muda wa wiki chache au miezi kadhaa.


Ugonjwa wa homa ya ini A


Ugonjwa wa homa ya ini aina ya kirusi hepatitis A umeanza mwaka 1973 uko Purcell ambapo binadamu pekee ndio walionekana kuwa hifadhi ya virusi hawa.


Kirusi Hepatitis A kipo katika Familia gani?


Kirusi cha Hepatitis A ni kimoja wapo kwenye familia ya virusi vya Picornaviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na umbile lenye pande 20 (icosahedral) na ukuta wenye strendi moja ya RNA.

Sifa za kirusi


Kirusi hepatitis A ni aina ya kirusi chenye strendi moja ya RNA. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Picornaviridae yenye sifa zifuatazo;

  • Huwa na virusi wadogo wenye ukubwa wa nautikomaili 22 hadi 30nm

  • Wana umbile lenye pande 20 (ikosahedro)

  • Wana ukuta wenye strendi moja ya RNA

  • Ganda lake la njee la seli halijafungwa

  • Wana kipenyo chanye urefu wa nautikomaili 30


Makundi ya familia ya Picornaviridae


Familia ya Picornaviridae ina genera tano ambazo ni; Enterovirus

  • Cardiovirus

  • Aphthovirus

  • Hepatovirus

  • Parechovirus


  • Genera zinazodhuru binadmau ni; Enterovirus

  • Hepatovirus

  • Rhinovirus


Utunzwaji wa kirusi


Kirusi hepatitis A hutunzwa na binadamu.


Uenezwaji wa kirusi


Kirusi hepatitis A kinaenezwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia;

  • Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono yake baada ya kutoka chooni

  • Kutumia maji ya kunywa yenye kirusi

  • Kujamiana na mtu mwenye maambukizi ya kirusi hepatitis A

  • Kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi ya kirusi hepatitis A


Vihatarishi vya maambukizi


Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Hepatitis A ni;

  • Kusafiri kwenda nchi zenye hali ya juu ya uambukizo ((Afrika, Asia, Mediterranean, Ulaya mashariki, Mashariki ya kati, amerika kusini na kati, Mexico na baadhi ya maeneo ya karibbean)

  • Mwanaume anayejamiana na mwanaume mwenzake

  • Kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi

  • Watu walio kwenye mazingira ya kazi yanayowakutanisha na wagonjwa wenye maambukizi ya kirusi hepatitis A

  • Watu walio kwenye taasisi kubwa

  • Wagonjwa wenye maambukizi ya kirusi cha UKIMWI


Dalili za maambukizi


Muda wa kuatema ni ndani ya wiki mbili hadi wiki sita. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumwambukiza mtu mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana. Dalili za ugonjwa wa Homa ya ini aina ya Hepatitis A ni;

  • Homa

  • Mwili kuchoka

  • Kupata manjano hasa machoni na kwenye ngozi

  • Kutapika

  • Kichefuchefu

  • Tumbo kuuma hasa upande wa juu wa kulia

  • Kupoteza hamu ya kula

  • Viungio vya mwili kuuma

  • Mwili kuwasha

  • Kupata mkojo wenye rangi nyeusi


Vipimo tambuzi


Vipimo muhimu kwa aliyeambukizwa kirusi Hepatitis A ni;

  • Kipimo cha picha nzima ya damu

  • Kipimo cha Nucleic Acid ya kirusi

  • Liver function test

  • Kipimo cha Seroloji

  • Ultrasonography

  • Kipimo cha biopsy ya ini

  • Kipimo cha ugandaji damu


Magonjwa yenye mfanano


Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa Homa ya ini A kutokana na maambukizi ya kirusi Hepatitis A ni;

  • Hepatitis E kali


Matibabu ya homa ya ini A


  • Mgonjwa anatakiwa apate mlo mzuri wenye virutubisho vyote

  • Mgonjwa atatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika

  • Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana

  • Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya kuzuia kutapika kama anatapika sana

  • Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya homa na maumivu

  • Mgonjwa atapandikizwa ini endapo ini lake litakuwa limeharibika.


Kinga


Inaweza kuwa ngumu kujikinga na kirusi huyu, hata hivyo kuna njia mbalimbali unazoweza kuchukua ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi;

  • Nawa mikono baada ya kutoka maliwato na unapogusana na mtu mwenye maambukizi haya (kinyesi, mate n.k)

  • Kunywa maji safi na salama

  • Kula vyakula vilivyoiva vema na kutoa mvuke

  • Kama unahudumia watoto kwenye vituo vya kulelea watoto, hakikisha unanawa mikono mara unapobadilisha nguo mtoto mmoja na kabla ya kwenda kwa mtoto mwingine

  • Usile vyakula vya mtaani

  • Safisha matunda kwa maji safi na salama ( unaweza tumia maji yaliyochemshwa)

  • Kupata chanjo


ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

Orodha kuu


  1. BMC. Hepatitis A Virus. https://bmcinfectdis.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12879-017-2555-x. Imechukuliwa 10/09/2021 2.

  2. MEDSCAPE. Hepatitis A Virus https://emedicine.medscape.com/article/177484-questions-and-answers. Imechukuliwa 10/09/2021

  3. FDA. Hepatitis A Virus (HAV). https://www.fda.gov/food/foodborne-pathogens/hepatitis-virus-hav. Imechukuliwa 10/09/2021

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 12:07:27

bottom of page