top of page

Mwandishi;

ULY CLINIC

Mhariri;

Dkt. Benjamin L, MD

6 Aprili 2020 20:09:29

Kirusi herpes simplex

Kirusi herpes Simplex

Kirusi herpes simplex, ni kirusi kilicho kwenye familia ya Herpesviruses, Familia hii ina virusi wengine ambao ni kirusi varicellazoster, Kirusi cytomegaly, kirusi Epstein–Barr na kirusi human herpes 8- kisababishi cha sakoma ya Kaposi’s.


Aina za virusi vya HSV


Kuna aina mbili za kirusi Herpes, HSV1 na HSV2. Aina hizi mbili hutokana na (i). Sehemu katika mwili iliyoathiriwa na kirusi na (ii) Antigeni ya kirusi. Maambukizi yanayosababishwa na kurusi aina ya kwanza yaani HSV1 hutokea maeneo ya juu ya kiuno na kirusi aina ya pili HSV2 husababisha maambukizi maeneo ya chini ya kiuno. Ugonjwa unaosababishwa na kirusi HSV2 hufahamika ka ugonjwa wa zinaa.


Magonjwa yanayosababishwa na kirusi HSV1


  • Gingivostomataitizi

  • Herpes labializi ya ghafla (kwa jina jingine homa ya baridi)

  • Keratokonjaktivaitizi(kerataitizi)

  • Ensefalaitizi haswa kwa watu wakubwa


Magonjwa yanayosababishwa na kirusi HSV2


  • Herpes ya maeneo ya siri

  • Ensefalaitizi ya vichanga

  • Meninjaitizi safi


Maambukizi ya HSV1 na HSV2 kwa pamoja


Maambukizi ya HSV1 na HSV2 huwezakusababisha ugonjwa uitwao erizima multifomi.


Sifa muhimu za kirusi


Kirusi HSV1 na HSV2 huwa ni vigumu kutofautishwa kwa umbo na mwonekano wake. Utofauti wake ni kwenye jinomu/DNA ya kirusi.


Kirusi HSV hutunzwa na nani?


Binadamu ni mtunzaji wa virusi hawa, hukaa na kujificha sehemu maalumu ya mishipa ya fahamu iitwayo ganglioni.


Kirusi HSV huzalianaje?


Kirusi mara anapoingia kwenye seli za binadamu, hufunguka kuta zake za nje kisha kuingiza jinomu yake kwenye seli. Kirusi huanza kujizalisha kwa kuagiza seli ya binadamu kuzalisha protini nyingi za kirusi, protini hizi huunganishwa ili kutengeneza kirusi wengine. Dawa inayotumika kutibu maambukizi ya kirusi hawa (acyclovir) hulenga kuharibu utengenezaji wa protini zinazounda kirusi huyu.


Uenezaji wakirusi


Kirusi HSV1 awali, huambukizwa kwa njia ya mate, wakati HSV2 huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Hivyo maambukizi ya HSV1 hutokea usoni au kinywani na HSV2 hutokea kwenye maeneo ya siri.


Hata hiyo kutokana na mabadiliko ya binadamu kuhusisha midomo kwenye tendo la kujamiana, maambukizi ya HSV1 yanaweza kutokea kwenye maeneo ya siri na HSV2 yakatokea kwenye maeneo ya kinywa kwa asilimia 10 hadi 20 ya wagonjwa.


Uzalianaji wa kirusi HSV


Kirusi mara anapoingia kwenye mwili, huanza kujizalisha kwenye eneo aliloingilia haswa kwenye ngozi laini kama ya uke na midomo au sehemu nyingine ya ngozi.


Mara baada ya kujizalisha huanza kutembea kuelekea kwenye ganglioni za nuroni haswa ganglioni ya traijemino kisha kulala hapo kwa muda wa miaka kadhaa kwa kirusi wa HSV1. Kirusi HSV1 hulala kwenye ganglioni zilizo maeneo ya Lamba na sakramu.


Ni nini huamsha virusi HSV waliolala mwilini?


Kirusi hawa huweza kuamshwa na mambo mbalimbali na kuleta ugonjwa wa homa, mambo hayo ni;


  • Jua kali

  • Mabadiliko ya homoni

  • Jeraha

  • Msongo wa mawazo

  • Homa na

  • Kuingia hedhi


Je vipele vya HSV huwa na virusi?


Malengelenge yanayotokana na virusi hawa huwa majimaji ambayo yana idadi kubwa ya virusi, protini pamoja na uchavu uliotengenezwa. Majimaji haya huwa ni si salama kwa sababu yakiguswa na mtu mwingine hupata maambukizi.


Maambukizi mapya


Mtu anaweza kupata maambukizi akapona na kisha akapata maambukizi mengine baadae.


Mwitikio wa kirusi kinga za mwili zinaposhuka


Kama kinga za mwili zimeshuka sana, kirusi HSV huamka na kusababisha mkanda wa jeshi. Soma zaidi kuhusu mkanda wa jeshi kwenye mada zingine katika tovuti hii.


ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

​

Orodha kuu


Rejea zamada hii;

  1. Warren Revinson. Herpesviruses. Chapisho la 14, kurasa 288-291 ISBN 978-0-07-184574-8 2.Kenneth M. Kaye. 

  2. MSD manual. Herpes simplex virus infections. https://www.msdmanuals.com/home/infections/herpesvirus-infections/herpes-simplex-virus-hsv-infections. Imechukuliwa 6.04.2020 3.

  3. CDC. Genital HSV Infections. https://www.cdc.gov/std/tg2015/herpes.htm. Imechukuliwa 06.04.2020

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 12:16:29

bottom of page