Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. benjamin L, MD
27 Septemba 2021 07:20:10
Kirusi human parainfluenza
Kirusi human parainfluenza ni kirusi kinachosababisha maambukizi katika mfumo wa upumuaji hasa kwa watoto. Maambukizi hayo ni kama mafua yenye homa, laryngotracheobronchitis , bronkolaitiz na nimonia.
Kirusi husababisha nini?
Kirusi hiki husababisha maambukizi kwenye mfumo wa upumuji.
Kirusi human parainfluenza kimeanza mwaka gani?
Tafiti za kwanza kuhusiana na kirusi Human parainfluenza kilionekana mwaka 1950.
Kirusi Human parainfluenza kipo katika Familia gani?
Kirusi Human parainfluenza ni kimoja wapo kwenye genus ya Respirovirus na familia ya Paramyxoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Sifa za kirusi
Human parainfluenza ni kirusi cha strendi moja ya RNA hasi. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya paramyxoviridae.Familia hii ina sifa zifuatazo;
Wana strendi moja ya RNA
RNA yake ni hasi
Ukuta wake wa njee ya seli umejifunga
Wana kipenyo cha 150-300nm
Wana mwili ambao haujajigawanya
Virusi wengine katika familia ya paramyxoviridae
Measles virus (surua)
Mumps virus
Kirusi respiratory syncytial
Genera za kirusi
Kirusi Human parainfluenza kimegawanyika katika genera mbili ambazo ni;
Respirovirus
Rubulavirus
Mtunzaji w akirusi
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Human parainfluenza hutunzwa na binadamu.
Uenezwaji wa kirusi
Kirusi Human parainfluenza kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Human parainfluenza kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia matone ya chafya, makohozi au hewa
Kugusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni
Kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi ya kirusi human parainfluenza
Vihatarishi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Human parainfluenza ni;
Watoto wenye lishe duni.
Mkusanyiko mkubwa wa watu.
Mtoto anayekosa maziwa ya mama
Wenye upungufu vitamin A
Mazingira
Dalili
Muda wa kuatema ni ndani ya siku moja hadi saba. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana. Dalili za kirusi human parainfluenza ni;
Joto kali la mwili (Homa)
Kikohozi
Coryza
Stridor
Retraction
Kupumua harakaharaka
Irritability
Vipimo vya utambuzi
Immunoglobulin G (1g G)
Immunoglobulin M (1g M)
Kuotesha virusi
Picha nzima ya damu
Picha ya shingo na kifua
Magonjwa yanayofanana
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na kirusi Human parainfluenza ni pamoja na;
Bronkaitiz
Kiusi Corona
Kupaliwa
Nimonia
Kirusi Respiratory syncytial
Adenovirus
Influenza
Nimonia ya Chlamydial
Coxsackieviruses
Maambukizi ya mycoplasma
Pediatric epiglotaitiz
Usaha kwenye retrofalinjo
Matibabu ya kirusi Human parainfluenza
Matibabu hulenga dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa yanayohusisha
Dawa kwa ajiri ya maambukizi ya bakteria
Vitamin A Suppliment
Maji ya kutosha kwa njia ya kunywa au mishipa
Dawa za kushusha homa (Panadol)
Dawa jamii ya corticosteroid na nebulizer kwa ajiri ya kupunguza michomo kinga na uvimbe kwenye mfumo wa hewa kama imeshukiwa
Oxygen kama kiwango chake cha oxygen chini ya kawaida
Kutolewa nguo kwa mtoto ili apate hewa ya kutosha
Kinga
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi
Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu.
Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye.
Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka.
Nawa mikono yako mara kwa mara
Epuka msongamano wa watu
Je kuna chanjo ya kirusi Human parainfluenza ?
Mpaka sasa hakuna chanjo ya kirusi Human parainfluenza .
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea za mada hii;
CDC. Human parainfluenza  virus. https://www.cdc.gov/human parainfluenza /index.html. Imechukuliwa 23/09/2021.
NCBI. Human parainfluenza  virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7171724/. Imechukuliwa 23/09/2021.
Medscape. Human parainfluenza  virus. https://emedicine.medscape.com/article/224708-overview. Imechukuliwa 23/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:06:56