Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Benjamin L ,MD
22 Septemba 2021 19:27:23
Kirusi Rota C
Kirusi Rota C ni kirusi kinasababisha maambukizi kwenye mfumo wa chakula na kusababisha homa ya kutapika na kuharisha (gastroentaraitiz) isiyo kali haswa kwa watoto wenye umri mkubwa.
Kirusi Rota C kimeanza mwaka gani?
Tafiti zinaonesha kuwa kirusi hiki kiligundulika mara ya kwanza kwa binadamu mwaka 1982 nchini Australia, United states, United kingdom, Finland, Japan, India, China, Malaysia na Latin America.
Kirusi Rota C kipo katika Familia gani?
Kirusi Rota C ni kimoja wapo kwenye genus ya Rota virus na familia ya Reoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi mbili ya RNA pia husababisha Homa ya matumbo kwa watoto.
Sifa za kirusi
Rota C ni moja ya kirusi cha strendi mbili ya RNA. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Reoviridae yenye sifa zifuatazo;
Wana RNA mbili
Ana Strendi mbili ya RNA
Ukuta wa juu ya seli yake umefunikwa kwa kapsidi mbili
Wana umbile la ringi
Wana kipenyo cha urefu wa 70nm
Genome yake ina vipande 11
Spishi za familia retroviridae
Familia ya reoviridae huwa na spishi ikiwa pamoja na Kirusi rota C ambao ni;
Kirusi rota A
Kirusi rota B
Kirusi rota C
Kirusi rota D
Kirusi rota E
Kirusi rota F
Kirusi rota G
Kirusi rota H
Kirusi rota IÂ
Spishi Zinazosababisha ugonjwa kwa binadamu ni;
Kirusi Rota A
Kirusi Rota B
Kirusi Rota C
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi Rota C hutunzwa na binadamu.
Kirusi Rota C kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi Rota C kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Kula chakula kilichoandaliwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono yake baada ya kutoka chooni
Kutumia maji ya kunywa au chakula chenye vimelea
Kushikana mikono na mtu mwenye maambukizi ambaye hakunawa mikono baada ya kutoka chooni
Watoto kugusa sehemu chafu pia kupeleka mdomoni bila kunawa mikono
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Rota C
Mtu yeyote ambayo hajapata chanjo ya kirusi Rota hasa watoto
Watoto wenye miaka 4 hadi 7
Watu ambao umri umeenda sana
Watu wazima wanaolea watoto wenye maambukizi
Dalili za gastroenteraitiz ya kirusi rota C
Dalili za ugonjwa wa homa ya matumbo huanza kuonekana ndani ya siku mbili baada ya mtu kupata maambukizi. Dalili hizo ni;
Kuharisha choo chenye majimaji na wakati mwingine damu kidogo
Kupata homa
Kutapika
Tumbo kuuma
Kukosa hamu ya kula
Mwili kukosa nguvu na kuchoka
Ishara zitakazoonekana kwa mgonjwa;
Mdomo kukauka
Miungurumo ya tumbo kuongezeka
Macho kuingia ndani
Ngozi ya mwili kuvutika
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kupungua uzito
Vipimo
Vipimo vinavyotumika katika utambuzi na matibabu ya maambukizi ya kirusi Rota C ni;
Kuotesha kirusi
Picha nzima ya damu
Kiwango cha madini kwenye damu
Kipimo cha haja kubwa
Latex agglutination
Enzyme immune Assay
Kipimo cha PCR
Magonjwa yanayofanana na maambukizi ya Rota C
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili za maambukizi ya Kirusi Rota C ni;
Amoebiasis
Giardiasis
Kuishiwa maji kwa mtoto
Maambukizi ya salmonella kwa mtoto
Matibabu ya Ugonjwa wa homa ya matumbo
Hakuna matibabu maalum kwa ajiri ya ugonjwa wa homa ya matumbo, ila mgonjwa anaweza pata yafuatayo;
Hakikisha njia ya hewa, upumuaji na mzunguko wa damu uko vizuri
Mtoto atapatiwa maji yenye sodium, potassium, chloride na calcium kwa njia ya mshipa
Mtoto anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika
Mtoto atapata panadol kwa ajiri ya maumivu na homa
Mtoto atapatiwa ORS kwaajiri ya kunywa
Mtoto atapatiwa Zinc ya watoto kupunguza kuharisha
Mtoto atapatiwa dawa za kuzuia kutapika kama anatapika sana
Kinga
Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;
Pata chanjo ya kirusi Rota A kwa wakati sahihi
Nawa mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote hasa mara baada ya kuingia na kutoka chooni
Osha mikono ya watoto mara kwa mara kwa maji safi na sabuni
Zingatia usafi kwa ujumla.
Je kuna chanjo ya kirusi Rota C?
Chanjo kwa ajiri ya kirusi Rota C ipo. Kuna chanjo aina mbili ambazo ni Rotateq inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 32 na Rotarix inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 24.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea zamada hii;
Sciencedirect. Rota C virus. https://www.sciencedirect.com/topics/medicine-and-dentistry/rotavirus. Imechukuliwa 21/09/2021.Â
NCBI. Rota C virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1234047/. Imechukuliwa 21/09/2021.Â
CDC. Rota C virus. https://www.cdc.gov/vaccines/pubs/pinkbook/downloads/rota.pdf. Imechukuliwa 21/09/2021.Â
Medscape. Rota C virus. https://emedicine.medscape.com/article/803885-overview. Imechukuliwa 21/09/2021.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:09:02