top of page

Mwandishi;

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri;

Dkt. Charles W, MD

27 Septemba 2021 07:24:18

Kirusi Rubella

Kirusi Rubella

Kirusi Rubella ni aina ya kirusi kinachosababisha ugonjwa wa Rubella. Kirusi hiki husababisha homa na vipele vinavyokuwa na rangi nyekundu vinavyoanzia usoni kuelekea kifuani.


Kirusi husababisha nini?

Kirusi hiki husababisha homa na vipele vinavyokuwa na rangi nyekundu vinavyoanzia usoni kuelekea kifuani.


Ugonjwa wa Rubella umeanza mwaka gani?

Ugonjwa wa Rubella ulianza mwaka 1962. Waliogundua ugonjwa huu walikuwa makundi mawili tofauti ambao ni Paul D. Parkman na wenzake pia Thomas H. Weller na Franklin A. Neva.


Kirusi Rubella kipo katika Familia gani?

Kirusi Rubella ni kimoja wapo kwenye genus ya Rubivirus na familia ya Togaviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi.


Sifa za kirusi

Kirusi Rubella ni kirusi cha strendi moja ya RNA hasi.Kirusi hiki ni familia ya virusi vya Togaviridae.Familia hii ina sifa zifuatazo;


  • Wana strendi moja ya RNA hasi

  • Wana umbile lenye pande 20 (icosahedral)

  • Ukuta wa njee wa seli ya bakteria imejifunga

  • Wana kipenyo cha 70nm


Makundi ya familia ya Familia

Familia ya Togaviridae imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni;

  • Alphavirus

  • Rubivirus


Virusi wengine walio kundi moja na Kirusi Rubella ni;

  • Eastern Equine encephalitis virus

  • Western equine encephalitis virus

  • Venezudan equine encephalitis virus

  • Chikungunya virus

  • River virus

  • Barmal forest virus


Kirusi hutunzwa na nani?

Kirusi Rubella hutunzwa na binadamu, nguruwe na farasi.


Kirusi Rubella kinaenezwa kwa njia gani?

Kirusi Rubella kinaenezwa kwa njia zifuatazo;


  • Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia vitonetone wakati mtu aliyeambukizwa anapopiga chafya, anapokohoa au anapopumua.

  • Wakati mwingine watu huambukizwa Rubella wanapogusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni.

  • Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.




Dalili za ugonjwa wa Rubella

Muda wa kuatema (incubation period) ni ndani ya siku kumi na nne mpaka siku ishirini na moja. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine hata kabla dalili hazijaonekana;


Dalili za ugonjwa wa Rubella ni;

  • Joto la mwili kupanda

  • Mwili kuchoka

  • Kuhisi baridi

  • Kichwa kuuma

  • Maumivu ya koo

  • Mafua

  • Vipele vinavyokuwa na rangi nyekundu vinavyoanzia usoni kuelekea kifuani

  • Kukosa hamu ya kula

  • Macho kuwa mekundu

  • Tezi kuvimba

  • Kichefuchefu


Vipimo

Vipimo vya Ugonjwa wa Rubella;


  • Picha nzima ya damu

  • Kuotesha virusi

  • Serological tests

  • Immunofluorescent assay

  • Latex agglutination test

  • Elisa test

  • Hemagglutination inhibition test


Magonjwa yanayofanana na maambukizi ya kirusi rubella

Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa Rubella ni;

  • Herpes Virus 6 infection

  • Measles

  • Parvovirus B19 Infection

  • Pediatric contact dermatitis

  • Pediatric cytomegalovirus infection

  • Pediatric enteroviral infection

  • Pediatric mycoplasma infection

  • Pediatric syphilis

  • Toxoplasmosis


Matibabu

Matibabu ya ugonjwa wa Rubella ni;


Hakuna matibabu maalumu ya ugonjwa wa Rubella ila mgonjwa anaweza kufanyiwa yafuatayo;

  • Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa.

  • Mgonjwa atapatiwa dawa kwaajiri ya homa na maumivu

  • Mgonjwa anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika

  • Mgonjwa anatakiwa anywe maji mengi ya kutosha

  • Mgonjwa anatakiwa apate chanjo kama bado hajapata chanjo


Kinga

Fanya yafuatayo ili uweze kujikinga na kirusi Rubella;

  • Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu.

  • Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye.

  • Pata chanjo ya Rubella kwa wakati sahihi.

  • Nawa mikono yako mara kwa mara.


Chanjo

Je kuna chanjo ya kirusi Rubella?


Chanjo kwa ajiri ya kirusi Rubella ipo na hutolewa mtoto akiwa na miezi 12 hadi miezi 15 pia atapata chanjo nyingine kwenye umri wa miaka 4 hadi miaka 6.




ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

​

Orodha kuu

​

Rejea za mada hii;

  1. SCIENCE DIRECT. Rubella Virus. https://www.sciencedirect.com/topics/neuroscience/togaviridae. Imechukuliwa 23/09/2021.

  2. MEDSCAPE.  Rubella Virus. https://emedicine.medscape.com/article/968523-overview. Imechukuliwa 23/09/2021.

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 12:05:27

bottom of page