Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Dawa nzuri ya maleria
Jibu kwa ufupi
Swali la mteja: "Habari daktari, ni dawa gani nzuri ya malaria?"
Jibu kwa ufupi: ALu (k.m. Coartem) kwa malaria isiyo kali iliyothibitishwa kwa kipimo; maliza dozi yote. Dalili za malaria kali – hospitali mara moja.
Maelezo
Malaria isiyo kali
Artemether-lumefantrine (ALu) – dawa ya kwanza Tanzania.
Dawa nyingine mseto za artemisinin (k.m. artesunate-amodiaquine, dihydroartemisinin-piperaquine) hutumika kwa maelekezo ya mtoa huduma.
Meza ALu pamoja na chakula au maziwa ili ifyonzwe vizuri.
Malaria kali
Sindano ya artesunate hospitalini, kisha ALu ya kumeza mgonjwa akiweza kumeza.
Quinine ni mbadala tu artesunate isipopatikana.
Wajawazito
ALu hutumika katika trimesters zote kwa malaria isiyo kali iliyothibitishwa.
Kama hawezi kutumia ALu au haonyeshi nafuu – rufaa kwa mtaalamu.
Malaria ujauzitoni ni hatari zaidi – nenda kituo cha afya mapema.
Nini cha kufanya
Pima malaria ukiwa na homa.
Maliza dozi yote hata ukijisikia vizuri.
Kunywa maji ya kutosha; paracetamol kwa homa.
Lala ndani ya chandarua chenye dawa kila usiku.
Malaria ikirudi haraka baada ya ALu – mwone mtoa huduma.
Dalili za hatari
Nenda hospitali mara moja ukiwa na:
Kuchanganyikiwa, kusinzia sana, kupoteza fahamu.
Degedege.
Kutapika kila kitu – huwezi kumeza dawa.
Kupumua kwa shida.
Mkojo mweusi au kidogo sana, macho kuwa ya njano.
Damu kutoka bila sababu.
Mjamzito au mtoto mdogo mwenye homa kali.
Lini umwone daktari
Homa haishuki siku 2 hadi 3 baada ya dawa.
Kipimo hasi lakini homa inaendelea – vipimo vingine.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Dawa gani bora ya malaria?
ALu kwa malaria isiyo kali, baada ya kupima.
2. Mjamzito wa miezi 2 anaweza kutumia ALu?
Ndiyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Taifa, katika trimesters zote.
3. Nimeze dawa ya malaria bila kupima?
Hapana, pima kwanza.
4. ALu inamezwa na nini?
Pamoja na chakula au maziwa.
5. Malaria kali hutibiwa vipi?
Kwa sindano ya artesunate hospitalini.
6. Nimemaliza dawa na homa bado ipo, nifanyeje?
Rudi kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:15
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.
World Health Organization. WHO guidelines for malaria. Geneva: WHO; 2024.
Ministry of Health Tanzania. National Guidelines for Diagnosis and Treatment of Malaria. Dodoma: MoH; 2021.

