top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Ibuprofen inatibu nini?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Hupunguza maumivu, homa na uvimbe. Baada ya chakula, kwa muda mfupi, kwa maelekezo ya mfamasia au daktari. Mjamzito au mwenye vidonda vya tumbo – paracetamol kwanza.



Maelezo


Hutumika kwa


  • Kichwa na kipandauso.

  • Meno.

  • Hedhi.

  • Misuli, viungo, mgongo, kuteguka.

  • Homa na maumivu ya mafua.

  • Baada ya upasuaji au jeraha.


Usitumie bila ushauri ukiwa na


  • Mimba ya wiki 20 au zaidi – huathiri figo za mtoto na maji ya chupa.

  • Dengue au homa yenye kutokwa damu.

  • Vidonda vya tumbo au damu kwenye kinyesi.

  • Ugonjwa wa figo, ini au moyo; presha isiyodhibitiwa.

  • Pumu inayozidi ukitumia aspirin au NSAID.

  • Unatumia dawa za kuzuia damu kuganda, steroid, au aspirin ya moyo.

  • Upungufu wa maji mwilini (kuharisha, kutapika).


Madhara


  • Kiungulia, tumbo kuuma, kichefuchefu.

  • Vidonda na damu tumboni.

  • Figo kuathirika.

  • Presha, moyo, kiharusi – kwa matumizi ya muda mrefu.


Nini cha kufanya


  • Inywe baada ya chakula na maji.

  • Usichanganye na NSAID nyingine (diclofenac, aspirin).

  • Watoto – kwa uzito, kwa maelekezo ya mtoa huduma tu.

  • Maumivu zaidi ya siku 3–5 – tafuta chanzo.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Kutapika damu au kinyesi cheusi.

  • Uvimbe wa uso, kupumua kwa shida, vipele vikubwa.

  • Maumivu ya kifua, udhaifu wa upande mmoja.

  • Mkojo kupungua sana.


Lini umwone daktari


  • Unahitaji dawa ya maumivu kila siku.

  • Maumivu ya tumbo au kiungulia vinavyoendelea.

  • Una ujauzito au unanyonyesha na unahitaji dawa ya maumivu.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Ibuprofen inatibu ugonjwa?

Hapana; hupunguza dalili tu.

2. Mjamzito anaweza kutumia?

Epuka kuanzia wiki 20; paracetamol ni chaguo la kwanza.

3. Ninywe kabla au baada ya chakula?

Baada ya chakula.

4. Inafaa kwa homa ya dengue?

Hapana; huongeza hatari ya kutokwa damu.

5. Naweza kuchanganya na diclofenac?

Hapana.

6. Mtoto anaweza kutumia?

Ndiyo kwa kipimo cha uzito, kwa maelekezo.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 17:07:37

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. U.S. Food and Drug Administration. FDA recommends avoiding use of NSAIDs in pregnancy at 20 weeks or later because they can result in low amniotic fluid. Silver Spring: FDA; 2020.

  2. World Health Organization. Dengue: guidelines for diagnosis, treatment, prevention and control. Geneva: WHO; 2009.

  3. Bhala N, et al. Vascular and upper gastrointestinal effects of non-steroidal anti-inflammatory drugs: meta-analyses of individual participant data from randomised trials. Lancet. 2013;382(9894):769–79.

  4. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page