Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37
Ishara ya mimba kutoka
Jibu kwa ufupi
Swali la mteja: "Je, inawezekana kutokwa na damu nyingi yenye mabonge bila maumivu na mimba bado ikaendelea kuwepo?"
Jibu kwa ufupi: Ndiyo, inawezekana. Ndiyo maana uthibitisho ni ultrasound au kipimo cha mkojo wiki 3 hadi 4 baadaye. Soma Utajuaje mimba imetoka baada ya misoprostol.
Maelezo
Ishara kwamba mimba imetoka
Damu nyingi zaidi ya hedhi, mabonge na tishu.
Maumivu ya kubana yanayopungua baada ya tishu kutoka.
Damu kupungua ndani ya siku chache hadi wiki 2.
Dalili za ujauzito (kichefuchefu, matiti kuuma) kupotea ndani ya wiki 1.
Mimba chini ya mwezi 1 – damu huweza kuwa kama hedhi nzito kidogo.
Kuthibitisha
Kipimo cha mkojo – baada ya wiki 3 hadi 4; mapema zaidi huweza kusoma chanya.
Ultrasound – huonyesha kama kizazi kiko tupu; usahihi hutegemea mpigaji.
Kipimo cha damu cha homoni (hCG) – kushuka kwake huthibitisha.
Nini cha kufanya
Pumzika, kunywa maji, kula vyakula vyenye madini chuma.
Usimeze dawa zaidi mwenyewe.
Nenda kituo cha afya kwa uchunguzi baada ya mimba kuharibika (PAC) – huduma ni ya siri.
Anza uzazi wa mpango.
Dalili za hatari
Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:
Kujaza pedi 2 kubwa kwa saa kwa saa 2 mfululizo.
Homa, uchafu wenye harufu mbaya.
Maumivu makali, hasa upande mmoja.
Kizunguzungu au kuzimia.
Lini umwone daktari
Kipimo bado chanya baada ya wiki 4.
Dalili za ujauzito zinaendelea – soma Dalili za utoaji mimba usio kamili.
Damu inaendelea zaidi ya wiki 2.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Damu nyingi yenye mabonge inamaanisha mimba imetoka?
Mara nyingi, lakini si kwa uhakika – thibitisha.
2. Nipime mimba lini kujua imetoka?
Wiki 3 hadi 4 baadaye.
3. Kipimo kimesoma chanya wiki 1 baada ya mimba kutoka, ni kawaida?
Ndiyo, homoni hubaki mwilini kwa wiki kadhaa.
4. Ultrasound inaweza kuthibitisha?
Ndiyo, inaonyesha kama kizazi kiko tupu.
5. Mkojo wa asubuhi ni bora kwa kipimo?
Ndiyo, una homoni nyingi zaidi.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 17:08:28
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Abortion care guideline. Geneva: WHO; 2022.
American College of Obstetricians and Gynecologists. Medication abortion up to 70 days of gestation. Practice Bulletin No. 225. Obstet Gynecol. 2020;136(4):e31–47.

