Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:43

Je, misoprostol na mifepristone ni salama kwa uavyaji mimba?
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Ni salama tu chini ya mtoa huduma aliyefunzwa. Usitumie mwenyewe. Una damu au maumivu baada ya mimba kuharibika – PAC inapatikana hospitali.
Maelezo
Kwa nini usitumie bila mtoa huduma
Mimba nje ya kizazi haitoki kwa dawa – huweza kupasuka na kuhatarisha maisha.
Mimba kubwa kuliko unavyodhani – hatari ya damu nyingi.
Dawa bandia zinauzwa mitaani.
Magonjwa kama upungufu wa damu, matatizo ya kuganda kwa damu yanahitaji uangalizi.
Matumizi mengine halali ya misoprostol
Kuzuia na kutibu damu nyingi baada ya kujifungua.
Kutibu mimba iliyoharibika (PAC) chini ya mtoa huduma.
Nini cha kufanya
Ukiwa na mimba isiyotarajiwa – ongea na mtoa huduma kuhusu chaguo zote na msaada.
Baada ya mimba kuharibika – anza njia ya uzazi wa mpango; soma Nani anaweza kutumia majira ya vichocheo viwili?.
Kipimo cha mimba hubaki chanya wiki 3 hadi 4 baada ya mimba kutoka – soma Mimba huonekana kwenye kipimo kuanzia siku ngapi?.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Damu nyingi – pedi 2 au zaidi kwa saa, kwa saa 2 mfululizo.
Homa, uchafu wenye harufu mbaya.
Maumivu makali ya tumbo, kizunguzungu au kuzimia.
Lini umwone daktari
Damu inaendelea zaidi ya wiki 2.
Dalili za ujauzito zinaendelea.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Misoprostol ni salama?
Chini ya mtoa huduma aliyefunzwa, ndiyo; bila uangalizi kuna hatari.
2. Naweza kununua dawa hizi dukani?
Hapana; zinahitaji mtoa huduma.
3. Uavyaji mimba ni halali Tanzania?
Kwa masharti finyu tu, kulinda maisha au afya ya mama.
4. PAC ni nini?
Huduma ya baada ya mimba kuharibika – ni halali na inapatikana hospitali.
5. Nitaenda hospitali nikiwa na damu nyingi, nitakamatwa?
Hapana; PAC ni huduma ya kawaida, usiogope kwenda.
6. Mimba nje ya kizazi inatoka kwa dawa hizi?
Hapana; ni hatari, inahitaji hospitali.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:13
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Abortion care guideline. Geneva: WHO; 2022.
Ministry of Health Tanzania. National post-abortion care (PAC) guidelines. Dodoma: MoH; 2015.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

