top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Sospeter B, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:43

Je, vipimo vya tezi dume ni vipi?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Dalili (IPSS), uchunguzi wa kidole, mkojo, PSA, figo na ultrasound. Mwone daktari ukiwa na dalili au ukiwa na miaka 50 au zaidi. Soma Chakula cha tezi dume.


Maelezo


Vipimo


  • IPSS – maswali 7 ya dalili; hupima ukali.

  • Uchunguzi wa kidole (DRE) – ukubwa, ugumu, uvimbe.

  • Mkojo – maambukizi, damu, sukari.

  • PSA – huongezeka kwa BPH, maambukizi na saratani; tafsiri kwa daktari.

  • Kreatinini – kuangalia figo.

  • Ultrasound – ukubwa wa tezi, mkojo uliobaki, figo.

  • Uroflowmetry – nguvu ya mkojo, kwenye vituo vikubwa.

  • Biopsy – PSA juu au tezi ngumu, kuthibitisha saratani.


Kabla ya PSA


  • Epuka kumwaga shahawa saa 48 na baiskeli ndefu.

  • Maambukizi ya mkojo hupandisha PSA – pima baada ya kutibiwa.


Nini cha kufanya


  • Punguza vinywaji jioni, kahawa na pombe.

  • Kojoa mara mbili (subiri kidogo kisha kojoa tena).

  • Taja dawa zako – za mafua huzidisha dalili.


Dalili za hatari


Hospitali mara moja ukiwa na:


  • Kushindwa kabisa kukojoa.

  • Damu nyingi kwenye mkojo.

  • Homa pamoja na maumivu ya kukojoa.


Lini umwone daktari


  • Kuamka kukojoa mara 2 au zaidi usiku.

  • Mkojo dhaifu au wa kukatika.

  • Maumivu ya mgongo au mifupa pamoja na dalili za mkojo.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Vipimo vya tezi dume ni vipi?

IPSS, uchunguzi wa kidole, mkojo, PSA, figo na ultrasound.

2. PSA ikiwa juu ni saratani?

Si lazima; BPH na maambukizi huipandisha pia.

3. Uchunguzi wa kidole unauma?

Hapana, ni usumbufu kidogo kwa sekunde chache.

4. Nianze kupima lini?

Ukiwa na dalili, au kuanzia miaka 50 (45 kama una historia ya familia) baada ya ushauri.

5. Ultrasound inaonyesha nini?

Ukubwa wa tezi na mkojo unaobaki.

6. Tezi dume kuvimba ni saratani?

Mara nyingi hapana; BPH si saratani.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:17

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. European Association of Urology. EAU guidelines on management of non-neurogenic male LUTS. Arnhem: EAU; 2024.

  2. Lerner LB, et al. Management of lower urinary tract symptoms attributed to benign prostatic hyperplasia: AUA guideline. J Urol. 2021;206(4):806–17.

  3. Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

bottom of page