Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kiasi cha maji ya kunywa kwa Siku: Kikokotoo
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Jaza taarifa zako na ubonyeze 'Kokotoa'. Kipimo rahisi: mkojo wa njano hafifu unaonyesha maji yanatosha. Soma Upungufu wa maji mwilini.
Maelezo
Jinsi ya kutumia
Weka uzito (kilo), jinsia, kiwango cha shughuli na hali ya hewa.
Chagua hali maalumu kama ujauzito au kunyonyesha.
Bonyeza 'Kokotoa' – matokeo ni makadirio, si amri.
Wanaohitaji maji zaidi
Hali ya joto, kazi za jua, mazoezi – ongeza glasi 2 hadi 4.
Homa, kuharisha, kutapika – ORS kwa kuharisha.
Wajawazito – karibu lita 2.3; wanaonyonyesha – karibu lita 2.7 (pamoja na chakula).
Wazee – hupoteza hisia ya kiu; wakumbushwe.
Wanaopaswa kufuata ushauri maalumu
Moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa sugu wa figo (dialysis), ini.
Kunywa maji mengi sana kwa muda mfupi kunaweza kushusha chumvi mwilini (hyponatraemia) – mfano wakati wa mashindano ya mbio.
Nini cha kufanya
Kunywa maji safi kidogo kidogo mchana kutwa.
Chagua maji badala ya soda na juisi za viwandani.
Vyakula vyenye maji – matunda (tikiti maji, machungwa, papai), mboga, supu, uji.
Beba chupa ya maji kazini au shuleni.
Dalili za hatari
Kiu kali, mkojo kidogo sana na mweusi, kizunguzungu, kuchanganyikiwa – hospitali.
Mtoto mwenye macho kuzama, kulegea, hakojoi.
Lini umwone daktari
Kiu kingi kisicho cha kawaida na kukojoa mara nyingi – pima sukari.
Una ugonjwa wa moyo au figo – uliza kiasi chako.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Mtu mzima anywe maji kiasi gani?
Karibu lita 1.5 hadi 2 za kunywa; jumla na chakula lita 2 hadi 2.5.
2. Chai na uji vinahesabiwa?
Ndiyo, vinachangia maji.
3. Mkojo wa njano sana una maana gani?
Mara nyingi maji hayatoshi.
4. Kunywa maji mengi ni hatari?
Kupita kiasi kwa muda mfupi kunaweza kuwa hatari.
5. Mjamzito anywe kiasi gani?
Karibu lita 2.3 kwa siku pamoja na chakula.
6. Mwenye figo dhaifu anywe kiasi gani?
Fuata ushauri wa daktari wako.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:23
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
European Food Safety Authority. Scientific opinion on dietary reference values for water. EFSA J. 2010;8(3):1459.
Institute of Medicine. Dietary Reference Intakes for Water, Potassium, Sodium, Chloride, and Sulfate. Washington DC: National Academies Press; 2005.
Popkin BM, D'Anci KE, Rosenberg IH. Water, hydration, and health. Nutr Rev. 2010;68(8):439–58.

