Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Mangwella S, MD
Dkt. Lugonda B, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:43

Kidonge cha calcium nyongeza
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Calcium ni salama na husaidia kuzuia kifafa cha mimba. Meza kama kliniki ilivyoelekeza, saa tofauti na vidonge vya chuma.
Maelezo
Vyanzo vya calcium kwenye chakula
Dagaa (wanaoliwa na mifupa yake), samaki wadogo.
Maziwa, mtindi, maziwa mgando.
Ulezi na uji wake.
Mboga za majani – mchicha, majani ya maboga, kisamvu.
Maharage, soya, ufuta, karanga.
Mambo ya kuzingatia
Calcium na chuma – angalau saa 2 kati yake.
Usimeze zaidi ya kiasi ulichoelekezwa – huweza kuleta choo kigumu.
Wenye mawe ya figo au matatizo ya figo – ushauri maalumu.
Nini cha kufanya
Hudhuria kliniki ya wajawazito na pima shinikizo la damu kila mahudhurio.
Kula dagaa, maziwa na mboga za majani kila siku.
Endelea na vidonge vya chuma na foliki.
Dalili za hatari
Hospitali mara moja ukiwa na:
Kichwa kuuma sana, kuona giza au nyota, maumivu chini ya mbavu kulia.
Uso na mikono kuvimba ghafla.
Degedege.
Lini umwone daktari
Choo kigumu sana au maumivu ya tumbo baada ya kuanza calcium.
Shinikizo la damu limepanda kliniki.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Calcium ni salama kwa mjamzito?
Ndiyo.
2. Inasaidia nini?
Kupunguza hatari ya kifafa cha mimba na kuzaa kabla ya wakati.
3. Nianze lini?
Kwa kawaida kuanzia wiki 20, kwa maelekezo ya kliniki.
4. Naweza kumeza na kidonge cha damu?
Hapana kwa wakati mmoja; tenganisha saa 2 au zaidi.
5. Vyakula vipi vina calcium?
Dagaa, maziwa, ulezi, mboga za majani.
6. Calcium inamdhuru mtoto?
Tafiti hazijaonyesha madhara.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:17:50
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. WHO recommendation: calcium supplementation during pregnancy for the prevention of pre-eclampsia and its complications. Geneva: WHO; 2018.
Hofmeyr GJ, et al. Calcium supplementation during pregnancy for preventing hypertensive disorders and related problems. Cochrane Database Syst Rev. 2018;10:CD001059.
Ministry of Health, United Republic of Tanzania. Standard Treatment Guidelines and National Essential Medicines List (STG/NEMLIT), 7th edition. Dodoma: Ministry of Health; 2026.

