top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:43

Kikokotoo cha idadi ya siku za mzunguko wa hedhi

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Weka tarehe 3 au zaidi za siku ya kwanza ya hedhi, kisha bonyeza "Kokotoa Mzunguko". Wastani wa siku 24–38 ni kawaida kwa mwanamke mzima. Soma Namna ya kufahamu urefu wa mzunguko wa hedhi.



Maelezo


Jinsi ya kutumia


  • Andika tarehe ya siku ya kwanza ya kutokwa damu kwa hedhi 3 au zaidi mfululizo.

  • Bonyeza "Kokotoa Mzunguko".

  • Utaona siku kati ya kila hedhi na wastani wake.


Mfano


  • Hedhi 1: 12/07/2025 → Hedhi 2: 15/08/2025 = siku 34.

  • Hedhi 2 → Hedhi 3: 17/09/2025 = siku 33.

  • Hedhi 3 → Hedhi 4: 16/10/2025 = siku 29.

  • Wastani ≈ siku 32 – kawaida; tofauti ni siku 5 – kawaida.


Kumbuka


  • Kikokotoo si njia ya kuzuia mimba wala kipimo cha ugonjwa.

  • Damu ya katikati ya mzunguko au baada ya tendo si hedhi – usiihesabu.


Nini cha kufanya


  • Andika tarehe zako kila mwezi kwenye kalenda au simu.

  • Andika pia siku za kutokwa damu na wingi wake.

  • Soma Siku za mzunguko wa hedhi.


Dalili za hatari


Mwone mtoa huduma haraka ukiwa na:


  • Hedhi kuchelewa na kipimo cha mimba ni chanya, pamoja na maumivu ya tumbo au damu.

  • Damu nyingi – kubadilisha pedi kila saa au kizunguzungu.


Lini umwone daktari


  • Mzunguko chini ya siku 24 au zaidi ya 38 mara kwa mara.

  • Tofauti ya zaidi ya siku 7–9 kati ya mizunguko.

  • Kukosa hedhi miezi 3 bila mimba.

  • Soma Mzunguko wa hedhi usio wa kawaida.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Mzunguko unahesabiwa kuanzia lini?

Siku ya kwanza ya hedhi hadi siku moja kabla ya hedhi inayofuata.

2. Mzunguko wa siku 32 ni wa kawaida?

Ndiyo, kwa mwanamke mzima siku 24 hadi 38 ni kawaida.

3. Nahitaji tarehe ngapi?

Angalau 3; zaidi ni bora.

4. Kikokotoo kinaweza kuzuia mimba?

Hapana.

5. Mzunguko wangu unabadilika kila mwezi, ni tatizo?

Tofauti ya hadi siku 7–9 ni kawaida.

6. Binti mdogo ana mzunguko wa siku 40, ni kawaida?

Ndiyo, katika miaka ya mwanzo baada ya kuvunja ungo.

7. Lini nimwone daktari?

Mzunguko ukiwa nje ya viwango mara kwa mara au kukosa hedhi miezi 3.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:21

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Munro MG, Critchley HOD, Fraser IS; FIGO Menstrual Disorders Committee. The two FIGO systems for normal and abnormal uterine bleeding symptoms and classification of causes of AUB in the reproductive years: 2018 revisions. Int J Gynaecol Obstet. 2018;143(3):393–408.

  2. American College of Obstetricians and Gynecologists. Committee Opinion No. 651: Menstruation in girls and adolescents: using the menstrual cycle as a vital sign. Obstet Gynecol. 2015;126(6):e143–6.

  3. Bull JR, et al. Real-world menstrual cycle characteristics of more than 600,000 menstrual cycles. NPJ Digit Med. 2019;2:83.

bottom of page