top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kikokotoo cha Umri wa Ujauzito: Wiki, Uzito wa Mtoto na Ushauri wa Lishe

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Weka tarehe ya siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho, bonyeza Hesabu. Kama tarehe hiyo haijulikani au mzunguko wako si wa siku 28, tumia umri kutoka ultrasound.



Maelezo


Jinsi ya kutumia


  • Weka tarehe ya kwanza ya hedhi ya mwisho – siku damu ilipoanza, si ilipoisha.

  • Bonyeza Hesabu.

  • Matokeo: wiki na siku za ujauzito, tarehe ya kujifungua, makadirio ya uzito, mchoro wa ukuaji (wiki 12 hadi 40), ushauri wa lishe na dalili za hatari.


Kukokotoa kwa mkono


  • Ongeza siku 7 kwenye tarehe ya kwanza ya hedhi ya mwisho, toa miezi 3, ongeza mwaka 1.

  • Mfano: hedhi ilianza 10 Januari 2026 – tarehe ya kujifungua ni karibu 17 Oktoba 2026.

  • Mzunguko mrefu (mfano siku 35) – tarehe husogea mbele siku 7.


Mipaka ya kikokotoo


  • Hakitumiki vizuri kama hukumbuki tarehe, mzunguko hauna mpangilio, ulikuwa kwenye vidonge au sindano, au unanyonyesha.

  • Uzito unaoonyeshwa ni wastani – mtoto wako anaweza kuwa mdogo au mkubwa kidogo.

  • Uzazi kati ya wiki 37 na 42 ni wa kawaida.


Nini cha kufanya


  • Anza kliniki kabla ya wiki 12 – ultrasound ya mapema huthibitisha umri.

  • Hudhuria kliniki angalau mara 8 (WHO).

  • Meza FEFO kila siku.

  • Kuanzia wiki 28 – fuatilia mtoto kucheza kila siku.


Dalili za hatari


Nenda kituo cha afya mara moja ukiwa na:


  • Damu ukeni.

  • Kichwa kuuma sana, kuona vibaya, uso au mikono kuvimba ghafla.

  • Maji kutoka ukeni.

  • Mtoto kucheza kidogo au kutocheza.

  • Homa, degedege, kupumua kwa shida.


Lini umwone daktari


  • Kikokotoo na ultrasound zinatofautiana zaidi ya siku 7 – fuata ultrasound.

  • Umepita wiki 41 bila uchungu.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Kikokotoo kinatumia tarehe gani?

Siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho.

2. Tarehe ya kujifungua ni sahihi kiasi gani?

Ni makadirio; wengi hujifungua kati ya wiki 37 na 42.

3. Sikumbuki tarehe ya hedhi, nifanyeje?

Tumia ultrasound ya mapema.

4. Mzunguko wangu ni siku 35, kikokotoo kinafaa?

Ongeza siku 7 kwenye tarehe; ultrasound ni bora.

5. Uzito wa kikokotoo ni wa mtoto wangu hasa?

Hapana, ni wastani wa watoto wa umri huo.

6. Ultrasound ya miezi 3 ni sahihi kiasi gani?

Kwa karibu siku 5 hadi 7.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:15

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. American College of Obstetricians and Gynecologists. Committee Opinion No. 700: Methods for estimating the due date. Obstet Gynecol. 2017;129(5):e150–4.

  2. World Health Organization. WHO recommendations on antenatal care for a positive pregnancy experience. Geneva: WHO; 2016.

bottom of page