top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kikokotoo: Uwezekano wa kushika mimba baada ya mimba kutoka

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Baada ya mimba kutoka, uwezo wa kushika mimba hurudi haraka. Kama hutaki mimba, anza uzazi wa mpango mara moja. Soma Siku salama baada ya kutoa mimba.



Maelezo


Jinsi ya kutumia


  • Weka tarehe mimba ilipotoka au kutolewa.

  • Weka tarehe ulizoshiriki tendo baada ya hapo.

  • Kikokotoo kitaonyesha siku zenye hatari na uwezekano kwa kila tendo.


Mambo ya kujua


  • Uovuleshaji wa kwanza mara nyingi wiki 2 hadi 4 baada ya mimba kutoka.

  • Hedhi ya kwanza mara nyingi wiki 4 hadi 6.

  • Kipimo cha mimba kinaweza kusoma chanya hadi wiki 4 kwa homoni ya mimba iliyotoka – soma Kupata ujauzito baada ya kutoa mimba.


Nini cha kufanya


  • Anza uzazi wa mpango siku ile ile – soma Uzazi wa mpango baada ya kutoa mimba.

  • Tendo bila kinga – P2 ndani ya siku 3 hadi 5.

  • Pima mimba wiki 3 baada ya tendo la mwisho bila kinga.


Dalili za hatari


  • Maumivu makali upande mmoja, kizunguzungu, damu nyingi au homa – kituo cha afya mara moja.


Lini umwone daktari


  • Kipimo bado chanya wiki 4 baada ya mimba kutoka.

  • Hedhi haijarudi wiki 6.

  • Mnataka mimba nyingine – ushauri wa muda unaofaa.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Naweza kushika mimba wiki 2 baada ya mimba kutoka?

Ndiyo, inawezekana.

2. Kikokotoo kinaweza kunihakikishia siku salama?

Hapana, ni makadirio tu.

3. Nianze uzazi wa mpango lini?

Siku ile ile au mara moja baadaye.

4. Nipime mimba lini?

Wiki 3 baada ya tendo bila kinga; kumbuka homoni ya mimba iliyotoka.

5. Nisubiri muda gani kabla ya kujaribu mimba nyingine?

WHO hushauri angalau miezi 6 baada ya mimba kutoka au kutolewa, kwa afya bora.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:08

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. World Health Organization. Abortion care guideline. Geneva: WHO; 2022.

  2. World Health Organization. Report of a WHO technical consultation on birth spacing. Geneva: WHO; 2007.

bottom of page