Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Lugonda B, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Kipimo cha Ultrasound kwenye Ujauzito
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Ultrasound ni salama. Ya kwanza kabla ya wiki 14 (au angalau kabla ya 24); ya viungo wiki 18–22; nyingine kwa sababu maalum. Usibadilishe tarehe ya kujifungua kwa ultrasound ya miezi ya mwisho. Soma Umri wa ujauzito.
Maelezo
Aina
Ya tumboni – kawaida; mapema hunywa maji kibofu kijae.
Ya ukeni – mimba changa; ni salama.
Doppler – mtiririko wa damu kwa mtoto anayekua polepole.
3D/4D – picha za kumbukumbu; si lazima.
Kwa wiki
Wiki 6–13 – mahali mimba ilipo, moyo, umri, mapacha.
Wiki 18–22 – viungo, kondo, maji, jinsia ikiombwa.
Wiki 28+ – ukuaji, mlalo, maji, kondo kuziba njia.
Majibu ya kawaida kuzungumzia
Kondo chini – mara nyingi hupanda; rudia wiki 32.
Maji kidogo au mengi – ufuatiliaji.
Mtoto mdogo kwa umri – ufuatiliaji wa ukuaji na Doppler.
Tarehe tofauti na hedhi – soma Ultrasound ya mimba.
Nini cha kufanya
Beba kadi ya kliniki na majibu ya zamani.
Uliza maswali kuhusu majibu.
Ultrasound haichukui nafasi ya kliniki za kawaida.
Dalili za hatari
Damu ukeni, maumivu makali, maji kutoka, mtoto kupunguza kucheza – hospitali mara moja.
Lini umwone daktari
Hujafanya ultrasound kufikia wiki 24.
Majibu yamekuchanganya.
Historia ya upasuaji au matatizo ya mimba iliyopita.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Ultrasound ni salama?
Ndiyo.
2. Ya ukeni ni salama kwa mimba?
Ndiyo.
3. Nifanye mara ngapi?
Angalau mara 1 kabla ya wiki 24; zaidi kwa sababu maalum.
4. Inaonyesha jinsia lini?
Mara nyingi wiki 18–22.
5. 3D ni bora?
Si lazima kitabibu.
6. Tarehe imebadilika?
Ya mapema ndiyo sahihi zaidi.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:10
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. WHO recommendations on antenatal care for a positive pregnancy experience. Geneva: WHO; 2016.
American College of Obstetricians and Gynecologists. Practice Bulletin No. 175: Ultrasound in pregnancy. Obstet Gynecol. 2016;128(6):e241–56.
Salomon LJ, et al. ISUOG Practice Guidelines (updated): performance of the routine mid-trimester fetal ultrasound scan. Ultrasound Obstet Gynecol. 2022;59(6):840–56.

