Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Lugonda S, MD
31 Oktoba 2026, 15:23:37

Majira yenye vichocheo viwili na kisukari
Jibu kwa ufupi
Jibu kwa ufupi: Kisukari peke yake si kizuizi. Kisukari cha muda mrefu au chenye madhara ya mishipa – epuka vidonge mchanganyiko na sindano ya projestini; chagua kitanzi, kipandikizi au vidonge vya projestini pekee.
Maelezo
Wasiotakiwa kutumia vidonge mchanganyiko
Kisukari cha zaidi ya miaka 20.
Madhara ya mishipa ya damu.
Madhara ya macho (retinopathy).
Madhara ya figo (nephropathy).
Madhara ya neva (neuropathy).
Pia: presha, uvutaji sigara, umri 35+ – soma Majira kwa mwenye kiharusi.
Kwa nini
Kisukari tayari huongeza hatari ya magonjwa ya mishipa; estrojeni huongeza zaidi hatari ya damu kuganda.
Tafiti (Cochrane 2014) zinaonyesha vidonge vya kisasa vina athari ndogo tu kwenye sukari – tatizo kubwa ni mishipa ya damu, si sukari yenyewe.
Njia salama
Kitanzi cha shaba – salama kabisa.
Kitanzi cha homoni, kipandikizi, vidonge vya projestini pekee – vinafaa kwa wengi.
Sindano ya projestini – haipendekezwi kwa wenye madhara ya mishipa.
Kondomu.
Nini cha kufanya
Mwambie mtoa huduma muda uliokaa na kisukari na madhara yoyote.
Dhibiti sukari, presha na lehamu.
Panga mimba – sukari ikidhibitiwa kabla ya mimba hupunguza kasoro kwa mtoto.
Dalili za hatari
Maumivu ya kifua, mguu mmoja kuvimba, udhaifu upande mmoja wa mwili ukiwa kwenye vidonge – hospitali mara moja.
Lini umwone daktari
Una kisukari na unatumia vidonge mchanganyiko – kagua kama vinakufaa.
Sukari inapanda tangu uanze njia mpya.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
1. Nina kisukari, naweza kutumia vidonge vya majira?
Kama huna madhara ya mishipa na kisukari si cha zaidi ya miaka 20, kwa wengi ndiyo, kwa ufuatiliaji.
2. Vidonge vya majira vinaleta kisukari?
Hapana.
3. Njia gani bora kwa mwenye kisukari?
Kitanzi au njia za projestini pekee kwa wengi.
4. Sindano ya Depo inafaa kwa mwenye kisukari?
Kwa wasio na madhara ya mishipa inaweza; wenye madhara – haipendekezwi.
5. Vidonge vinapandisha sukari?
Kidogo sana kwa vidonge vya kisasa.
Imeandikwa:
2 Aprili 2026, 19:07:15
ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Medical eligibility criteria for contraceptive use. 5th ed. Geneva: WHO; 2015.
Lopez LM, Grimes DA, Schulz KF. Steroidal contraceptives: effect on carbohydrate metabolism in women without diabetes mellitus. Cochrane Database Syst Rev. 2014;(4):CD006133.
Gourdy P. Diabetes and oral contraception. Best Pract Res Clin Endocrinol Metab. 2013;27(1):67–76.

