top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Imeboreshwa:

Dkt. Mangwella S, MD

Dkt. Salome A, MD

31 Oktoba 2026, 15:23:37

Manii huishi kwa muda gani kwenye kizazi?

Jibu kwa ufupi


Jibu kwa ufupi: Hadi siku 5 ndani ya kizazi. Tendo siku 5 kabla ya yai kutoka linaweza kuleta mimba. Soma Siku za kupata mimba mzunguko wa siku 28.


Maelezo


Muda wa kuishi


  • Ute wa shingo ya kizazi siku za uovuleshaji – hadi siku 5.

  • Ukeni (mazingira ya tindikali) – saa chache.

  • Nje ya mwili – hufa zikikauka, dakika chache.

  • Maji ya bwawa au bafu – hazifiki ukeni kwa njia hii.


Maana yake


  • Tendo kabla ya siku za hatari bado linaweza kuleta mimba – soma Siku 14 baada ya kumaliza hedhi.

  • Yai huishi saa 12 hadi 24 tu baada ya kutoka.

  • Siku za kushika mimba ni karibu 6 kwa kila mzunguko.


Nini cha kufanya


  • Unayetafuta mimba – tendo kila siku 1 hadi 2 kuanzia siku 5 kabla ya uovuleshaji.

  • Unayezuia mimba – tumia njia ya uzazi wa mpango; P2 ndani ya saa 72 baada ya tendo bila kinga.

  • Andika tarehe za hedhi kukadiria siku za hatari.


Dalili za hatari


  • Hedhi imechelewa na maumivu makali upande mmoja wa tumbo – hospitali mara moja.


Lini umwone daktari


  • Mmejaribu mwaka 1 bila mimba.

  • Unataka kuchagua njia ya uzazi wa mpango.


Maswali yanayoulizwa mara kwa mara


1. Manii huishi muda gani ndani ya mwanamke?

Hadi siku 5.

2. Naweza kupata mimba tendo la siku 4 kabla ya uovuleshaji?

Ndiyo.

3. Manii huishi muda gani nje ya mwili?

Dakika chache zikikauka.

4. Manii kwenye nguo zinaweza kuleta mimba?

Hapana kwa kawaida.

5. Yai huishi muda gani?

Saa 12 hadi 24.

6. Siku za hatari ni ngapi?

Karibu 6 kwa mzunguko.

Imeandikwa:

2 Aprili 2026, 19:07:17

ULY CLINIC inashauri usitegemee au kufuata ushauri wowote uliyoona kwenye makala hii bila kuwasiliana kwanza na daktari wako. Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya matibabu, hakikisha umepata ushauri rasmi kutoka kwa daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.

​

Makala hii ni ya kielimu tu na haitumiki kama mbadala wa matibabu ya daktari.

Rejea za mada hii:

  1. Wilcox AJ, Weinberg CR, Baird DD. Timing of sexual intercourse in relation to ovulation. N Engl J Med. 1995;333(23):1517–21.

  2. Morrison AI. Persistence of spermatozoa in the vagina and cervix. Br J Vener Dis. 1972;48(2):141–3.

  3. World Health Organization, Johns Hopkins CCP. Family planning: a global handbook for providers. 2022 ed. Geneva: WHO; 2022.

bottom of page